Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kuzialika nchi za Afrika Mashariki maonyesho Nanenane

Morogoro. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde amesema serikali inatarajia kukuza wigo wa maonyesho yajayo ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuzialika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ili kubadilishana ujuzi na taaluma wanazotumia katika kilimo chao.

 Silinde amesema hayo mkoani Morogoro baada ya kutembelea maonyesho ya 30 ya Nanenane Kanda ya Mashariki ambapo amesema ili kuongeza tija kwa wakulima katika maonesho hayo ni wakati sasa wa kuyaalika mataifa ya Rwanda, Uganda na Burundi ili kujua taaluma wanayotumia katika kilimo chao.

Amesema hata hiyo itawawezesha watanzania kujifunza mbinu za kilimo zinazotumiwa na mataifa hiyo, na itachagiza ukuaji katika uzalishaji kwa shughuli kilimo.

"Kwanza niwapongeze viongozi wanaosimamia Maonesho haya kwa Kanda ya Mashariki kwa namna ilivyoandaa, niseme tu Maonesho yajayo serikali itayaalika mataifa ya Rwanda, Uganda na mataifa mengine kushiriki pia ili kujua taaluma wanayotumia katika kilimo chao,"amesema Silinde

Aidha Naibu Waziri huyo amewataka wauzaji wa viuatilifu kuhakikisha wanatoa takwimu na taarifa zenye kutoa majawabu sahihi kwa wakulima na wafugaji ili ziweze kuleta tija katika uzalishaji.

Amesema wakulima na wafugaji wanapopatiwa majawabu yenye kujibu maswali yao kwa usahihi, wakaelishwa vyema namna ya matumizi sahihi ya viuatilifu kutachagiza katika uzalishaji na tija itaonekana.

"Kwa mfano mfugaji ukamuonyesha kwa vitendo, akajifunza kwa kuona faida za ufugaji bora, tija inayopatikana, itamuongezea uelewa zaidi kuliko kumwambia kwa maneno, ili aachane na ufugaji wa mazoea ng'ombe nyingi tija kidogo," amesema Silinde.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Mifugo kutoka Halmashauri ya Chalinze, Corman Herman amesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto katika utoaji wa elimu ya matumizi ya viuatilifu kwa baadhi ya wahitaji.

Amesema tabia ya kushikilia matumizi ya viuatilifu visivyo ruhusiwa kitaalamu imekuwa ni moja ya changamoto, ambapo matumizi ya dawa za asili kwa baadhi ya watu umekuwa kukichangia kutofikiwa malengo