Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yajipanga kutatua udumavu kwa watoto

Muktasari:

Wizara ya Kilimo imesema kupitia wataalamu wao watafanya utafiti mbalimbali ili kuzalisha mbegu bora zenye virutubisho zitakazotatua changamoto ya lishe nchini.

Dar es Salaam. Wizara ya Kilimo imesema kupitia wataalamu wao watafanya utafiti mbalimbali ili kuzalisha mbegu bora zenye virutubisho zitakazotatua changamoto ya lishe nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde amesema hayo alipokutana na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe kwa lengo la kujadili jinsi ya uzalishaji wa mbegu zitakakazokuwa na virutubisho zitakazosaidia kutatua changamoto ya wananchi za kupata lishe bora.

Mavunde amesema wizara hiyo kupitia taasisi za utafiti wa Kilimo wana wajibu wa kuhakikisha wataalamu wao wanakuja na aina mbalimbali za mbegu zilizoweza kupatiwa virutubisho kibaiologia Kwa lengo la kuondoa changamoto ya lishe nchini.

Amesema Serikali ina mkakati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wanatatua changamoto ya upatikanaji wa lishe bora ya wananchi.

"Wizara tunaunga mkono kwa sababu tunayo programu ya kulisha watoto shuleni lengo letu tutahakikisha kuwajengea lishe bora kwa watoto chini ya miaka mitano ili kujenga Taifa lenye imara watakaokuwa na uwezo wa kuchangia katika kulijenga Taifa kiuchumi.

"Tunafahamu changamoto kubwa suala la udumavu na Tanzania ni kati ya nchi ambayo imeathirika na suala la udumavu hivyo Serikali imekuja na mkakati katika mpango wa kitaifa na uzalishaji wa mbegu kupitia virutubisho vya kibaiologia.

Amesema wajibu wa Serikali hasa ugunduzi wa mbegu ambazo zitakuwa na madini ya chuma na zinki hasa kwenye maharagwe kutatua suala la lishe.

Mwakilishi wa Shirika linaloshughulika na Kilimo Tanzania (Agra), Viane Rweyendela amesema wamekutana wadau wanaoshughulikia masuala ya lishe Kwa lengo la kutatua upatikanaji wa mbegu zenye virutubisho vya kibaiologia.

Rweyendela amesema Shirika hilo limekuwa likisaidia katika miradi ya chakula hasa Tanzania tunaongelea upatikanaji wa chakula bora cha lishe ambapo wanazungumzia upatikanaji wa mbegu  zenye virutubisho.

Mkurugenzi wa taasisi inayoshughulika na mradi wa upandaji wa maharagwe yenye lishe kutoka nchini Kenya (The Rockefeller), Betty Kibaara amesema mradi huo unasaidia kukuza maharagwe yaliyoongezewa lishe bora kwa ajili ya watoto na akina mama.

"Lengo letu kuwafikia wanafunzi 400 kwa kuwa maharagwe ni muhimu na yanasaidia kuongeza rutuba kwenye udongo," alisema Kibaara.