Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaongeza bajeti ya maofisa ugani kwa asilimia 94

Serikali yaongeza bajeti ya maofisa ugani kwa asilimia 94

Muktasari:

  • Serikali imeongeza bajeti ya maofisa ugani kutoka Sh600 milioni hadi Sh11 bilioni mwaka 2021 kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa na maofisa hao ili kuleta kilimo chenye tija nchini.

Dodoma. Serikali imeongeza bajeti ya maofisa ugani kutoka Sh600 milioni hadi Sh11 bilioni mwaka 2021 kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa na maofisa hao ili kuleta kilimo chenye tija nchini.

Bajeti hiyo inahusisha kwa kiasi kikubwa uboreshaji wa zao la kimkakati la alizeti linalotoa tani 273,683 kwa mwaka.

Hata hivyo idadi hiyo ya uzalishaji ni pungufu kwani Serikali inahitaji mafuta ya kula tani 650,000 hivyo kufanya zao hilo kuwa na upungufu wa uzalishaji wa tani 37,317 na kuilazimu Serikali kutumia zaidi ya Dola milioni 171.72 kwa mwaka kuagiza mafuta ya kula kutoka nje.

Hayo yamesemwa na Waziri wa kilimo Adolf Mkenda wakati akifungua mafunzo rejea ya kilimo bora cha alizeti kwa maofisa ugani kwa awamu ya kwanza yaliyofanyika wilaya ya Mpwapwa jijini hapa.

Asema katika kutatua changamoto ya upungufu wa mafuta ya kula nchini, Serikali imepanga kutoa mafunzo rejea kwa maafisa ugani nchi nzima ikihusisha mikoa inayolima zao hilo ambapo kwa awamu ya kwanza wameanza na wilaya ya Mpwapwa, Kongwa, Bahi na Sekretarieti ya Mkoa.

Amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi katika Ofisi ya Rais (Tamisemi) wamepanga kuwawezesha maofisa ugani kupeleka elimu kwa wakulima ili kutatua tatizo la uzalishaji mdogo na usio na tija kw alengo la kuokoa fedha zianztumika kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi.

“Mafunzo haya yameanza kwenye kilimo cha alizeti ikiwa ni mkakati wa kuongeza uzalishaji wenye tija kwenye zao hili. Viwanda vyetu vinafanya kazi siku mbili tatu vinafungwa kwasababu kwa kukosa malighafi, hivyo mafunzo haya yatasaidia kuongeza uzalishaji,” amesema.

Aidha amewaagiza maafisa ugani kuwa na mashamba darasa kama sehemu ya wakulima kujifunza kwa mfano huku Serikali ikiwapa kipaumbele cha kuwapa usafiri na vifaa kazi ili kuleta matokeo chanya kwenye mkakati huo.