Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatakiwa kuweka wazi ripoti za kamati zinazoundwa

Muktasari:

Serikali ya Tanzania imetakiwa kutoa matokeo ya kamati zinazoundwa kuchunguza majanga mbalimbali yanayotokea nchini ikiwa ni pamoja na kuweka wataalamu wa majanga husika ili kuja na suluhisho la kudumu.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imetakiwa kutoa matokeo ya kamati zinazoundwa kuchunguza majanga mbalimbali yanayotokea nchini ikiwa ni pamoja na kuweka wataalamu wa majanga husika ili kuja na suluhisho la kudumu.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Novemba 16, 2022 na wadau mbalimbali  wakati wa mjadala wa TwitterSpace uliolenga kuzungumzia matokeo ya ripoti zinazoundwa kuchunguza majanga yanakidhi matarajio ya wananchi na nini kifanyike.

Mjadala huo unaendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na Mkurugenzi wa Rich Out Tanzania, Kumbusho Dausen amesema, “Tume zinaundwa ili kutumia kodi za wananchi au ni vinginevyo? Serikali iwe sikivu kwa madiwani, na viongozi wengine, watu wamepiga kelele bungeni mara kadhaa Serikali imekaa kimya.

Ndege ya Precision Air iliyopata ajali Ziwa Victoria Novemba 6, 2022 na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 24 ikitolewa kwenye maji.

“Kuna tume iliundwa na waziri mkuu baada ya soko la Kariakoo kuungua nini kimetokea, tuache kutafuta tatizo ndipo kuundwe tume ninadhani tuangalie nini kifanyike, huwezi kuzuia majanga yasitokee je, yanapotokea tuna uwezo wa kuyadhibiti? Kariakoo ipo jirani na makao makuu ya Zimamoto lakini hakuna kilichofanyika,” amesema.


Dausen amesema njia pekee ya kutatua matatizo kwanza ni kusikiliza ushauri wa wananchi, wanaharakati, wanasiasa na wadau wengine.


Amesema Watanzania wana uhuru wa kutoa maoni yao ili majanga yasiweze kutokea huku akitolea mfano wa ajali ya ndege ya Bukoba ni Serikali kushindwa kuwajibika licha ya baadhi ya wananchi kutoa maoni yao wakiwemo wabunge wa Bunge la Tanzania.


Mchangiaji wa mada hiyo Marwa Warioba amesema Serikali imekua inaunda tume huku ikijua tatizo ni nini na viongozi hawawajibiki kuangalia kudhibiti matukio haya yasitokee.


“Wanatakiwa kuhakikisha wanafuatilia tatizo lisitokee na siyo kuunda tume na kuzikalia ripoti ni kitu kinachopoteza rasilimali za Tanzania vijana na watu wanakufa pasipo hatia,” amesema.


Warioba amesema tume zinazoundwa basi zishirikishe wataalamu wa kamati husika

Naye Ansikari Victor amesema, “ukiangalia tangu kuanza kuundwa kwa kamati hizi hazijawahi kuleta matokeo chanya na mbaya zaidi wachunguzi au wanaohusika na hizi tume hawako huru kwahiyo tuna changamoto hiyokubwa.

“Ninakumbuka ile ajali ya moto iliyotokea Morogoro, waziri mkuu aliagiza iundwe tume ya uchunguzi lakini hadi leo hatujawahi kupata matokeo yoyote na tume zilizoundwa ni nyingi tu lakini kilichotokea baada ya hapo hatujui.”