Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatoa kauli mzabuni mfumo wa kuratibu mwenendo wa mabasi

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditike  (kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kulia) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu walipohudhulia kikao cha Bunge, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuz

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imesema mzabuni aliyetekeleza mradi wa mfumo wa kuratibu mwenendo wa mabasi (VTS) alipatikana ka ushindani. Mfumo huo huwezesha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za basi likiwa safarini.Taarifa hizo ni pamoja na mwendokasi, mahali basi lilipo, matukio ya ajali na jina la dereva.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema mzabuni aliyefanya kazi ya kuweka mfumo wa kuratibu Mwenendo wa Mabasi (VTS) alipatikana kwa njia ya ushindani, kwamba mfumo huo uligharimu Sh2.4 bilioni zilizotokana na mapato yake.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Juni 21, 2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditike wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalum (Chadema), Cecilia Paresso aliyetaka kujua umegharimu kiasi gani, sababu za mzabuni kutopatikana kwa ushindani kwa kufuata sheria za manunuzi na nani anayeusimamia.

Akijibu swali hilo, Nditiye amesema, “Mzabuni aliyefanya kazi hii ni kampuni ya Bsmart Technologies ya Malaysia akishirikiana na kampuni ya Computer Center ya nchini na alipatikana kwa njia ya ushindani.”

“Mfumo huu unasimamiwa na kuendeshwa na Sumatra (Mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa Majini na Nchi Kavu) kupitia kituo maalum kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Sumatra imeingia mkataba na kampuni ya Tera kwa ajili ya kufunga vifaa hivyo kwenye magari,” ameongeza