Seuwasa waanza oparesheni nyumba kwa nyumba kubaini wezi wa maji Sengerema

New Content Item (2)
New Content Item (2)

Sengerema. Mamulaka ya Maji Safi na Usafi Mazingira mjini Sengerema (Seuwasa) inaendelea na msako wa nyumba kwa nyumba kubaini watu waliojiunganishia maji kinyemela na kuikosesha Mamulaka hiyo mapato na kusababisha Shirika la umeme Tanzania Tanesco kuwakati umeme na kuleta adha kwa wananchi.

Oporeshen hiyo iliyoanza Machi 3 mwaka huu ilifanikiwa kumukamata mmiliki wa shule ya Tumaini English medium, Experancia Maunde kukutwa amejiunganishia maji kinyemela kwenye shule yake na kupatia hasara Mamulaka hiyo.

Kutoka na hali hiyo mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mkoa wa mwanza, Emmanuel Kipole aliagiza  vyombo vya dola kumusweka ndani mmiliki wa shule ya Tumaini English medium iliyoko Wilayani Sengerema,  Experancia Maunde kwa kosa la kukutwa amejiunganishia maji  kinyemela kwenye shule hiyo kinyume na utaratibu.

Kipole amesema watu wanajiunganishia maji kinyemela na kuisababishia harasa Serikali nisawa na wahujumu uchumi hivyo wanatakiwa kushughurikiwa.

"Nataka aswekwe ndani olewenu  mkiuke maagizo yangu ocd tekeleza na nipate taarifa " amesema Kipole.

Mkurugenzi wa Mamulaka ya maji Safi na usafi wa mazingira mjini Sengerema (Seuwasa), Robert Lupoja amesema wamebaini kuwa amechimba tanki la majin chini  ya Aridhi ambacho hujaza maji na linawezo wa kaa na ndani ya miezi sita hivyo bila maji kuisha na maji  hayo hayahesabiwi kwenye mita.

Meneja biashara Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mjini Sengerema Valentine Mazebele amesema walifanya zoezi hilo kwenye shule hiyo kutoka na mmiliki wa shule hiyo kuleta bili ndogo ya Sh200,000 huku shule zingine zinaleta bila ya kuanzia Sh1milinioni ndipo walipoamua kwenda na kubaini wizi huo.

Mmoja wa wananchi Wilayani Sengerema, Anna Simoni amesema watu waliojiunganishia maji kinyemela wako wengi hivyo oparesheni inatakiwa kuwa endelevu.