Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheria ya leseni za biashara kuboreshwa

Muktasari:

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeanza mchakato wa mabadiliko na maboresho ya baadhi ya vipengele vya sheria ya leseni za biashara sura namba 208.

Dar es Salaam. Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, uchumi na mwenendo wa biashara, Serikali imeanza mchakato wa maboresho ya sheria ya leseni za biashara sura namba 208.

Huu ni mwaka wa 50 tangu sheria hiyo itungwe mwaka 1972, hivyo maendeleo ya sekta ya biashara yamesababisha haja ya mabadiliko yake.

Akizungumza kuhusu mabadiliko ya sheria hiyo leo Septemba 14, Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andew Mkapa alisema hatua hiyo itajibu changamoto zinazojitokeza sasa.

“Kumekuwa na mabadiliko ya ulimwengu na sheria ilitungwa wakati ule kulingana na mahitaji yaliyokuwepo, lakini kwa sasa mambo yamebadilika inabidi tuwe na sheria inayoendana na sasa,” amesema.

Amesema mabadiliko hayo yametokana na pamoja na mambo mengine kuibuka kwa biashara za mtandao ambazo awali hazikuwepo hivyo sheria iliyopo haisemi chochote kuzihusu.

Amesema kwa sasa sheria hiyo inatekelezwa na BRELA na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo pia ndizo zenye mamlaka ya kutoa leseni hizo.

Kulingana na Mkapa, ukongwe wa sheria hiyo uliosababisha kuacha baadhi ya vipengele katika sekta ya biashara kwa sasa ndiyo sababu ya kubadilishwa kwake.


Amebainisha kuwa kikosi kazi kiliundwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa ajili ya kuandaa mapendekezo na sasa maoni yanakusanywa kutoka kwa wadau ili kuratibu mabadiliko hayo.

Sheria hiyo iliyorekebishwa mara 31 tangu kutungwa kwake, amesema ipo kimya kuhusu baadhi ya mambo ikiwemo wajibu wa anayepewa leseni.

 “Sheria imeruhusu ukaguzi lakini haijaeleza nini kinapaswa kukaguliwa kwa hiyo kila mkaguzi akifika kwa mfanyabioashara anakagua kitu chake hii inasababisha mkanganyiko,” ameeleza.

Hata hivyo, amesema kwa sababu sheria haipaswi kuwa mgando, ndio maana mchakato wa mabadiliko yake umeanza sasa.