Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shule zatakiwa kubuni mbinu za kimaendeleo ikiwemo kuzalisha vipaji

Muktasari:

  • Kamishna wa Skauti Wilaya ya Moshi, Emerensiana Mbena, amezitaka shule mbalimbali nchini kubuni njia zitakazo wawezesha siyo tu kufanya vizuri kitaaluma, kubolesha miundombinu lakini pia kuibua vipaji vya wanafunzi, na hivyo kuwa miongoni mwa shule bora.

Moshi. Kamishna wa Skauti Wilaya ya Moshi, Emerensiana Mbena, amezitaka shule mbalimbali nchini kubuni njia zitakazo wawezesha siyo tu kufanya vizuri kitaaluma, kubolesha miundombinu lakini pia kuibua vipaji vya wanafunzi, na hivyo kuwa miongoni mwa shule bora.

Kamishna huyo ameyasema hayo hayo katika mbio za hisani za kilomita 10 na kilomita tano zilizoandaliwa na shule ya sekondari ya St Mary Goreti, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuadhimisha Jubilee ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

“Kwa kweli St Mary Goreti mmedhihirisha kuwa ninyi sio wazuri kwenye elimu tu, bali hata kwenye michezo. Mbio za leo zimefanyika kwa weledi mkubwa na tumeona jinsi gani kuna vipaji hapa,” amesema Mbena na kuongeza;

“Natoa wito kwa shule zingine ziige mfano huu, kwa kubuni njia mbalimbali za kujiletea maendeleo... St Mary Goreti wanaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake na wamebuni njia tofauti za kuhamasisha uchangiaji katika harambee ya kufanikisha jubilee hii, mojawapo ikiwa ni mbio na matembez.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Abraham Mikumi, amesema shule hiyo wameonyesha mfano mzuri wa kuigwa ili kukuza vipaji hasa katika mchezo wa riadha.

“Tunawashukuru kwa kutushirikisha maana tunaweza kupata vipaji vitakavyokuzwa na kulitumikia Taifa katika mashindano mbalimbali. Hii ni shughuli kwa ajili ya kuchangisha fedha lakini pia kuna kipengele cha mashindano,” amesema Mikumi.

Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo pia amewapongeza wadhamini wa mbio hizo wakiwamo Kilimanjaro Water na Kampuni ya Simu ya TIgo kwa kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa ufanisi.

Makamu Mkuu wa shule hiyo, Cleopha Saritha, amesema walichagua kufanya mbio kama namna ya kuimarisha afya na kuhamasisha wananchi kuhusu harambee hiyo inayolenga kukusanya Sh600 milioni kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo kabla ya sherehe mwakani.

Mbio hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Ushirika Moshi (MoCU), zilikusanya zaidi ya washiriki zaidi ya 900 wakiwamo wanafunzi, wazazi, walimu na wananchi wa kawaida.