Simu yasimamisha kesi ya kina Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyopo Ubungo Mawasiliano jijini Dar es Salaam, jana. Picha na Michael Matemanga


Muktasari:

  • Simu ya mkononi iliyoita wakati kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu ikiendelea imesababisha Jaji kuahirisha kesi hiyo kwa muda na kwenda chemba kujadiliana na mawakili wa pande zote uamuzi wa kuchukua juu ya mwenye simu hiyo.

Dar es Salaam. Simu ya mkononi iliyoita wakati kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu ikiendelea imesababisha Jaji kuahirisha kesi hiyo kwa muda na kwenda chemba kujadiliana na mawakili wa pande zote uamuzi wa kuchukua juu ya mwenye simu hiyo.

Simu hiyo ya mtu ambaye ni miongoni mwa waliokuwa mahakamani kusikiliza kesi hiyo, iliita leo Ijumaa Januari 14, 2022 wakati kesi hiyo ikiendelea ambapo Jaji Joachim Tiganga alimuamuru mwenye simu kutoka nje huku akiahidi kulitolea uamuzi baadaye.

Wakati simu hiyo ikiita, Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala alikuwa anamhoji shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka Gladys Fimbari ambaye ni mwanasheria wa kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mikononi ya Airtel PLC Tanzania.

Ikiendelea kuita huku Jaji akiwa anamtazama, mtu huyo ambaye alikuwa amekaa benchi la pili nyuma ya bechi la mawakili wa Serikali alitumia muda kuzima simu hiyo bila mafanikio.

Bada ya muda mfupi, mfuasi huyo aliamuriwa kusalimisha simu kwa Jaji kisha kutolewa nje ya ukumbi wa mahakama chini ya ulinzi wa askari wanne.

Kabla ya kutolewa nje, wakili wa Serikali Mwamizi Robert Kidando alisimama na kuieleza Mahakama kuwa mtu huyo alikuwa anarekodi mwenendo wa kesi na kuiomba Mahakama imuamuru aisalimishe simu hiyo.

Hata hivyo baada ya muda Jaji Tiganga alimruhusu wakili Kibatala kuendelea kumuhoji shahidi huku akiahidi kulitolea uamuzi baadaye.

Baada ya upande wa utetezi na wa mashtaka kumaliza kumhoji shahidi huyo wa tisa, upande wa mashtaka ulimuomba Jaji kuahirisha kesi hiyo mpaka Jumatatu Januari 17 ili kuendelea na shahidi mwingine.

Ombi la upande wa mashtaka liliridhiwa lakini kabla ya Jaji kuahirisha aliwaita mawakili wa pande zote ofisini kwake ili kujadili suala hilo.

Baada ya muda mfupi mahakama ilirejea na Jaji kutoa uamuzi wa jambo hilo huku akisema

“Tuliahirisha kesi hii kwa muda kwa ajili ya kujadili suala lililojitokeza hapa mahakamani, baada ya majadiliano hayo, hekima imetumika na amerudishiwa simu yake,” amesema Jaji Tiganga na kuendelea

“Hivyo tumekubaliana pande zote mbili, kuwa mtu huyu hataruhusiwa kuingia katika ukumbi wa Mahakama kusikiliza Proceedings ya kesi hii,” ameeleza na kuongeza

“Naahirisha kesi hii hadi Januari 17, 2022, saa 3:00 asubuhi itakapoendelea na naelekeza upande wa mashtaka waje na shahidi na washtakiwa wote wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa Magereza. Niwatakie siku njema. High Court!!!!!!!”

Leo upande wa utetezi katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, namba 21 ya mwaka 2021, inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, ulikuwa unamalizia kumuuliza maswali shahidi wa tisa ambaye alitoa ushahidi wake jana Alhamisi.

Mbali na Mbowe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire Hassan (mshtakiwa wa kwanza) Adamu Hassan Kasekwa (mshtakiwa wa pili) na Mohamed Abdillahi Ling'wenya (mshtakiwa wa tatu).


Hapa ni mtiririko mzima wa kesi hiyo ilivyoendelea leo;


Washtakiwa wameshafikishwa katika ukumbi wa Mahakama

Mawakili wa pande zote nao wameshaingia

Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza shauri hilo ameshaingia

Mawakili wa pande zote nawajitambukisha

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando: Kesi hii imekuja kwa ajili ya upande wa utetezi kuhoji shahidi

Wakili Kidando: Hivyo sisi tupo tayari

Wakili Kibatala: Na sisi tupo tayari

Jaji: Shahidi upo chini ya kiapo

Shahidi huyo anaendelea kuhojiwa na wakili wa utetezi John Mallya

Mallya: Ni sahihi Cash Out ni pesa kutoka kwa wakala?

Shahidi: Ni mhusika mwenye namba anapokwenda kutoa pesa kwa wakala.

Mallya: Sasa Shahidi interest yangu ni muamala uliotoa jana katika ushahidi wako wa Julai 20, 2020, hiyo aliyetumia Sh500, 000 alienda akatoa Sh300, 000 ni sawa

Shahidi: Ni sahihi.

Mallya: Hiyo pesa iliyobaki baada ya kutoa Sh300, 000 alifanyia nini?

Shahidi: Sifahamu.

Mallya: Kuna ile pesa Sh500, 000 aliyoitumia Denis Urio ilitoka kwa wakala? Au

Shahidi: Hiyo pesa haikutumwa kutoka kwa wakala bali ilitoka kwenye line ya Tigo.

Mallya: Hivi line ya Airtel inauzwa sh ngapi bei yake?

Shahidi: Sh500.

Mallya: Kuna regulation ya mwaka 2015 inavyofanya usimamizi wa Simcard, je Unafahamu?

Shahidi: Naifahamu.

Mallya: Sasa kupitia regulation hiyo, unafahamu line ya Halfan Bwire imeuzwa kwa mtu mwingine, Unafahamu?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Sasa nyie mmeuza line ya Bwire kwa Sh500 na pesa zilizokuwepo kwenye line yake.

Mallya: Sasa line ya Bwire ilikuwa na hela, mmezipeleka wapi?

Shahidi: Tumeziweka kwenye Collection Account.

Mallya: Kwa hiyo Airtel mna fedha za ugaidi kwenye Collection Account?

Wakati Mallya anaendelea kumhoji shahadi.. ghafla amesimama wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla na kuongoa.

Hilla: Maneno ya Mallya kuhus fedha za ugaidi kuingia kwenye Collection Account sio maneno mazuri na

Hilla: Tunaomba Mahakama imwelekeze Wakili Mallya, ajikite kuuliza maswali..

Jaji: Mallya nilishakuulizaga hayo maneno mengine unayoyasema unataka tuyaweke wapi?

Jaji: Ni staili yako hiyo kila wakati huwa unaitumia na wakati mwingine unazungumza mambo mengine ambayo hayapo kwenye Proceeding za kesi.

Jaji: Mimi napenda umuulize maswali na sio kumsimulia.

Mallya: Sawa Jaji nimekuelewa.

Jaji: Haya endelea.

Mallya: Haya Airtel mmeuza line yake na pesa mmechukua.

Mallya: Sasa huyu mshtakiwa (Bwire) leo hii akitaka kujitetea kuhusiana na line yake akipiga inapokea mtu mwingine anayeitwa Godson Mnuru, je mlitoa ufafanuzi.

Shahidi: Hapana.

Shahidi: Kwa utaratibu line ya simu yoyote ikikaa miezi mitatu bila kutumika anapewa mtu mwingine.

Mallya:  Namba ya Bwire imesajiliwa na Godson Mnuru, na imesajiliwa Januaria 2021? Sasa wakati wewe unaandaa taarifa iliyoombwa na vyombo vya usalama hukuona line ya Bwire imesajiliwa kwa jina jingine?

Shahidi: Siwezi kutoa jibu.

Mallya: Kwa miezi 10, namba ya simu ya Bwire, ingekuwa Deactivated?Ndio: Ndio.

Mallya amemaliza kumhoji shahidi.

Kwa sasa ni zamu ya wakili Peter Kibatala anayemtetea Freeman Mbowe.

Kibataka: Gazeti la The Citizen la Suturday January 12, 2019, liliandika kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo timu yake iliongozwa na Waziri Profesa Kabudi, walifanya mazungumzo na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ili kuongeza hisa kutoka asilimia 40 hadi asilimia 49, Ni sahihi?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Kwa hiyo Serikali ya Tanzania ni mabosi wako?

Shahidi: Sio mabosi wangu.

Kibatala: Kwa hiyo wale wakurugenzi walioteuliwa na Airtel, Ni mabosi wako?

Shahidi: Sio mabosi wangu.

kibataka: Wewe unaripoti kwa nani?

Shahidi: Naripoti kwa Legal Counsel.

Kibatala: Ni kweli Gladys tangu umeajiriwa mwaka 2013 hadi sasa hujui unaripoti kwa Legal Counsel?

Kibatala: Huyo Legal Counsel anaripoti kwa nani?

Shahidi: Kwa Mkurugenzi

Kibatala: Na huyo Mkurugenzi anaripoti kwa nani?

Shahidi: Bodi ya Wakurugenzi.

Kibatala: Unafahamau mteja wako Freeman Mbowe ni kiongozi wa chama siasa Cha Upinzani?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Unafahamu wakili leo umekuja kutoa ushahidi kwenye kesi gani?

Shahidi: Mpaka nifanyi reference.

Kibatala: Nakuuliza tena unafahamu umekuja kutoa ushahidi kuhusu kesi gani inayomkabili mteja wako kule Airtel?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala:  Umekuwa Airtel kwa miaka 8 hujui umekuja kutoa ushahidi kwenye kesi gani?

Shahidi: Economic Crime.

Kibatala: Ni kweli kabla ya kuwa Airtel ulikuwa The Guardian?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibalata: Umekuja kutoa ushahidi au umekuja kushindana na sisi?

Shahidi: Kutoa ushahidi.

Kibatala: Imeandikwa barua ya kutoa taarifa na ilikufikia tarehe ngapi?

Shahidi: Julai 2, 2020.

Kibataka: Sasa baada ya kupokea barua hiyo uliochukua juhudi zipi kumlinda mteja au mlichukua juhudia zipi za kubalance huyu mteja wako?

Shahidi: Niliombwa kutoa taarifa na Mamlaka husika hivyo, nisingweza kuacha kutoa.

Kibatala: Hivi kampuni ya Airtel mliwandikia barua yoyote Polisi ..ili kujiridhisha na barua ya ombi ya Jeshi la Polisi wakitaka taarifa za wateja wenu?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Kuna kitu chochote kilichowazuia kufanya hivyo?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Hivi kulikuwa na uharaka gani wa Airtel kutoa taarifa za mteja kwa siku hiyo hiyo baada ya kuletewa barua ya ombi na jeshi la Polisi? Bila kuchunguza barua hiyo?

Kibatala: Hivi si huwa mnatakiwa kujiridhisha kwa barua zote zianakuja hapo kwenu? Ni sahihi?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Sasa zaidi ya kuona nembo ya Jeshi Polisi, barua Pepe na namba za simu, je kuna authenticate yoyote uliyoichukua ili kumlinda mteja wako wa Airtel?

Shahidi: Barua yenyewe ilikuwa inajitosheleza.

Kibatala: Kwa hiyo hukufanya?

Kibatala: Mpaka unafanya hivyo, ulimfahamu Inspekta Swilla anachunguza na kuandika maelezo ya kesi ya ugaidi na sio makosa ya mtandao?

Shahidi: Alinaindika maelezo.

Kibatala: Swilla alikuambia au hakukuambia wakati anachukua maelezo yako?

Shahidi: Hakuniambi

Kibatala: Wewe uliandika maelezo ya nini?

Shahidi: Zile taarifa nilizotoa, ambazo kwa mujibu barua ya Julai 2, 2020 ni tuhuma za jinai.

Kibatala: Hizo tuhuma za jinai ulikuwa unazifahamu?

Shahidi: Nilikuwa sizifahamu na hazinihusu.

Kibatala: Hiyo barua kutoka Polisi uliyoitoa kama kielelezo ni kopi au original?

Shahidi: Original

Kibatala: wewe unafanya kazi masjala ya Polisi?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Ndio maana nilikuuliza hapa unafahamu chain of Custody? na authentics, ukasema hufahamu

Kibataka:  Nyie Airtel mna Kitengo kinaitwa risk?

Shahidi: Sijaelewa swali lako.

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji, kwa suala hili ni kitengo gani kina deal na taarifa hii?

Shahidi: Kitengo cha sheria ndio kina deal.

Kibatala: Taarifa hizi za kutoa taarifa za mteja, Bodi inajua? Au haijui?

Shahidi: Rudia swali.

Kibataka: Ni sahihi au sio sahihi, taarifa hizi lazima Bodi ipewe hata kama Mkurugenzi hawezi kuzisoma yeye lakini lazima apewe taarifa?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Kwenye Ushahidi wako ulisema mna kampuni yenu Ina Firewalls, sasa mwambia Mheshimiwa Jaji ni firewalls gani mnayotumia Airtel.

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mliwahi kupokeq barua ya kuwa Freeman Mbowe yuko nje ya nchini na namba zake hizi hapa kwa ajili ya kufanya uchunguzi?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Iwapo Jeshi la Polisi lingewafahamisha Mbowe anajihusisha na vitendo vya kigaidi mngefuatikia namba zake?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kama Airtel mliwahi kufahamu Mbowe anatuhumiwa kwa masuala ya ugaidi?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Nyie kama Mbowe baada ya Julai 2, 2020 alikuwa anafanya kazi zake uraiani, je mliwahi kunote au kugundua kitu chochote?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Majukumu yenu katika kuripoti kama mmeambiwa huyu mtu anatuhumiwa kwa ugaidi?

Shahidi: Kuna vigezo tunavyoangalia.

Kibatala: Mimi nataka unitajia hata kimoja.

Shahidi: Siwezi kutaja kwa sababu ni siri.

Kibatala: Sawa kama siri okay.

Kibatala: Hamjawahi kusikia namba ya Mbowe inapiga kengele, alifanya miamala mikubwa?

Shahidi: Ndio hatujawahi kusikia kengele ikilia.

Kibatala: Kama hufahamu hata aina ya sever ya Airtel Bado unataka tuamini Kuwa hizi data haijachezewa

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba Sever ya Airtel ni ya aina fulani

Shahidi:  Hapana sikumwambia

Kibatala:  Je ulimwambia kuwa hizo saver zinakuwa upgraded lini

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Twende eneo lingine

Kibatala: Hizi system zote kuna watu wanazi mantain pamoja na kuzifanyia auditing

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba kuna internal auditors

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Nyie mna external auditor au hamna.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Nilisikia unazungumzia kuhusu Firewalls, kama ukuta for protection

Kibatala: Nyie si reporting authority?

Kibatala: Miamala ya tarehe 20 Julai 2020, zinahusisha namba gani na namba gani.

Shahidi: Ni 780900174 ambayo ituma Kwemda 787555200

Kibatala: Kwa hiyo hizo namab zinaanza na 7 na Siyo Sifuri

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Namba ambazo zipo katika kielelezo cha polisi na hizo, ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba ndiyo namba hiyo hiyo.

Shahidi: Si kutolea ufafanuzi

Kibatala: Unakubaliana na mimi kuwa kuna utofauti katika kielelezo P20 hizo namba hazianzi na sifuri lakini katika barua ya maombi zinaanza na sifuri,

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ambapo tunasema hukumfafanulia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nilisikia mnasema kuwa kuna Collection Akaunti au Wallet sijui nini

Shahidi: Unaweza kuita Wallet

Kibatala: Ni ya kampuni gani

 Shahidi:  Ni wallet ya Tigo

Kibatala: Wewe ni mtu sahihi kuzungumzia wallet ya Tigo?

Shahidi: Ndiyo naweza kuzungumzia

Kibatala: Kati yako wewe na mtu wa Tigo nani yupo competent kuzungumzia originating namba ya Tigo

Shahidi:  Ni mtu wa Tigo

Kibatala: Katika barua yako ya tarehe 02 Julai 2020 hukutoa maelezo yoyote

Shahidi: Ni kweli sikutoa

Kibatala: Transactions ya chini yake umesema ni namba ya Agent, Je unamfahamu.

Shahidi Hapana simfahamu

Kibatala: Airtel mnadasajili namba za Agent na mna file lake, Je ni kweli

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je Hilo file lipo hapa Mahakamani ilitujue kama ana uhusiano na Mbowe

Shahidi: Hapana halipo Mahakamani

 Kibatala: Katika barua yako ya 02 Julai 2020 uliwaambia polisi juu ya huyu Wakala

 Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Nikitumiwa namba yangu ya Airtel siwezi kumtuma house girl, akifika kwa Wakala anitumie namba niweze kutoa fedha hiyo

Shahidi: Haiwezekani

Kibatala: Kwa hiyo nikimtuma amtu aende kwa wakala wangu kutoa pesa na nikatoa bila mimi kuwepo pale siwezi kutoa pesa, haya niambie kwa sheria gani inayokataza

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Angalia katika taarifa ya namba ya Mbowe, tarehe 20 July 2020, mnasema kuwa alituma Sh 500,000 kwa Denis Urio

Shahidi: Hakuna muamala humu wa hiyo Sh 500,000.

Kibatala:  twende kielelezo namba 20, Nitafutie tarehe 22 July 2020 kuna mihamala miwili ambayo namba ya Freeman Mbowe ilituma pesa kwenda kwa Denis Urio au Khalfani Bwire either Sh 190,000 au 199,000

 Shahidi: Hakuna Miamala hiyo.

Wakati Kibatala akiendelea kuhoji shahidi…. simu imeita ndani ya ukumbi wa Mahakama ya mmoja wa wafuasi wa Chadema huku akijaribu kuizima bila mafanikio.


Hata hivyo wakati akiendelea kuizima bila mafanikio, Jaji alikuwa akimtazama, ndipo wakili Kibatala alipomtaka atoke nje ili kesi iweze kuendelea.

Lakini kabla ya mtu huyo kutoka nje kwa ajili ya kwenda kuizima, wakili wa Serikali Mwamizi Robert Kidando amesimama na kuieleza Mahakama kuwa mtu huyo anakuwa anarekodi mwenendo wa kesi.

Mfuasi huyo ambaye alikuwa amekaa benchi la pili nyuma ya bechi la  mawakili wa Serikali..alitumia muda mwingi kuzima simu hiyo bila mafanikio.

Kidando: Tunaomba asalimishe simu mbele ya mahakama na awe chini ya ulinzi kwa muda wote huu tunapendelea na ushahidi.

Mtu huyo jinsia ya kiume amesalimisha simu na kisha kutolewa nje ya ukumbi wa Mahakama chini ya ulinzi wa askari Polisi wanne.

Hata hivyo mtu huyo kabla ya kutoka nje ya ukumbi wa Mahakama, Kibatala alimuelekeza amuombe radhi Jaji na yeye kufanya hivyo.

Kibalata: Mheshimiwa Jaji kuna siku hapa Mahakama ilitoa uamuzi kuhusiana na shahidi wa upande wa mashtaka kukutwa na diary na simu akiwa kizimbani.

Kibatala: Mimi naona hayo ni mambo ya kawaida, asamehewe na sijui wakili wenzangu Kidando kama ana ushahidi wa hicho alichosema.

Kibatala: Mimi naomba Mheshimiwa Jaji tuendelee na kesi.

Jaji: Endelea Kibatala ... Lakini kuhusu hii suala hili la simu tutalitolea maamuzi baadae.

Jaji: Lakini akitoka nje na simu yake ananiachia mimi.. hapa? Alihoji Jaji.

Jaji: Mimi nashauri awepo katika maeneo haya haya ya mahakama asiende mbali.

Wakili Kibatala anaendelea kumkoji shahidi huyo wa upande wa mashtaka.

Kibatala:  Primary source ya taarifa ya mteja ambazo zinakuwa reflected katika KYC zipo NIDA ndiyo maana mna retrieve kutoka NIDA

 Shahidi: Sawa sawa

 Kibatala: Na wewe unafanya kazi NIDA

 Shahidi: Hapana

Kibatala: Na wewe hukutoa chochote kutoka NIDA

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakili wa Airtel nilisikia kuwa uliitwa Polisi kuwa ukaandike maelezo yako.

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kama uliyaandika kwa nia njema, na yalikuwa ya kweli, kwanini hutaki Kuyatoa mahakamani hapa?

Shahidi: Siyo kwamba sitaki kuyatoa

Kibatala:  Ndiyo sasa nakuuliza kwa nia njema kama kweli uliyaandika chini ya Mungu, kwanini usitoe

Shahidi: Jana hapa mahakamani kuna uamuzi ulitoka kuwa nisitoe.

Jaji: Mr Kibatala jana Mtobesya alisema kuwa mlikubaliana kuwa kama Jopo mna withdraw.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji kwa Heshima na taathima ni kweli Wakili mwingine akifanya Cross examination mimi siruhusiwi kuhoji hilo Jambo?

Jaji: Yeye Mtobesya alisema kuwa mlikubaliana "Sisi ni Jopo" na kwa bahati mbaya leo hayupo hapa mahakamani.

Kibatala: Kama ikiwezekana naomba utusomee ulicho rekodi

Jaji: Hapana sisomi, kwani wewe jana hukusikia?

Kibatala: Basi Mheshimiwa Jaji sitaki kubishana na mahakama, na nitaomba kuishia hapo.

Baada ya Kibalata kumaliza kumhoji shahidi wa upande wa mashtaka, kwa sasa ni upande wa mashtaka kuhoji shahadi kuhusiana na maswali aliyohijiwa na mawakili wa upande wa utetezi kwa kusawazisha hoja.

Ananza Wakili wa Serikali Mwandamizi, Jenitreza Kitale anasimama na kufanya reexamination.

Kabla ya kuanza kumhoji shahidi, wakili Kitale anaieleza.mahakaka wa breck kwa sababu wana maswali mengi ya kuhoji shahadi.

Ombi hilo linapingwa vikali na mawakili wa utetezi na kudai kuwa kesi hiyo iendelee.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji tunapinga wenzetu ku-breack kwa sababu tumegundua hawana shahidi mwingine, hivyo waendelee tu kumfanyia cross examination in chief shahidi ili tukimaliza tuwe tumemaliza tuondoke.


Mahakama inaridhia ombi la Kibatala na Jaji kueelekeza Wakili kumhoji shahidi.

Kitale: Shahidi jana uliulizwa kuhusu taarifa ya KYC taarifa za Msajili  hazionekani katika hiyo taarifa, Ni kwanini labda?

 Shahidi: Ni kweli haionekani lakini hizo taarifa zipo na zikihitajika zinaweza kuletwa Mahakamani

Wakili Mallya: Mheshimiwa Jaji Objection, taarifa kuwa zipo katika Mfumo wa Usajili zikihitajika zinaweza kuletwa Mahakamani si sawa na hii ni taarifa mpya.

Kilale:  Maoni yetu ni explanation, na kwa upande wetu sisi hatuwezi kuzuia shahidi kueleza jambo.

Jaji: basi eleza katika namna ambayo hatoleta jambo jipya.

Kitale: Shahidi jana uliulizwa kwamba Katika Taarifa Yako Msajili haionekani, Kwa nini ipo hivyo.

Shahidi: Mfumo ndiyo ulivyo lakini endapo zitahitajika zitaletwa.

Kitale: Umeulizwa kuhusu namba ya Simu Ikiwa Dormant, haitumiki na kwamba Airtel wamemuuzia mtu mwingine anaitwa GODSON MNURU, Ukasema huwezi kueleza mpaka uone Nyaraka, Ni sahihi au sio sahihi?

Shahidi: Ni kweli nilitaka anithibitishe jina, kwa sababu nisingeweza kujibu kabla sijathibitisha.

Kitale: Uliulizwa kuhusu Wakala kuwa hukutoa details za Wakala aliye fanya huo muamala wa Sh 300 000, ni Kwanini ?

Shahidi:  Mheshimiwa Jaji sikuwa nimeombwa taarifa hiyo.

Shahidi:  Kuna vitu vingi tunaangalia katika kutoa taarifa, kuna Sheria zinaniruhusu kufanya hivyo na Sheria siyo moja, kwa hiyo Sheria inaniruhusu kufanya hivyo pale ninapo takiwa kutoa taarifa

Kitale: Kuna Taarifa kwenye Kielelezo namba 17 kuhusu neno "kanda" Kimoja Kina Neno hilo Kanda Kimoja Hakina, Ieleze Mahakama kwanini ilijitokeza hivyo

Shahidi: Nilivyosema hiki kimetolewa katika mfumo wakati mteja taarifa zake zina tolewa katika mfumo wa NIDA hivyo taarifa nilizo wasilisha ndiyo zilivyoletwa.

Kitale:  Mheshimiwa Jaji maswali yangu yameisha, naomba nimkaribishe mwenzangu wakili Kidando, aendelee.


Kidando: Gladys jana uliulizwa  maswali kuhusiana kielelezo namba 20, ambacho ilikuwa na Taarifa ya Mihala ya Namba 0787 555200 na ukasema Taarifa za mihamala mwingine za Airtel, ukaulizwa umechukua hatua gani kulinda Taarifa za Wateja Wengine 19 ambazo hazikuwa zimeombewa lakini zinaomekana, Je Ulimaanisha Nini

Shahidi: Kwanza Taarifa za Wateja ziliombwa Kupitia Utaratibu wa Kisheria, katika taarifa hizi tunaona Mtumiaji anafanya Mihamala na namba zingine, hatuna Uwezo wa kufanya changes zozote kwenye Taarifa hizo.

Mallya: Mheshimiwa Jaji  hizo ni fact mpya.

Jaji: Alisema jana kuwa wana extract na kuprint, hawezi kuzichanganua

Mallya: Sawa mheshimiwa Jaji.

Wakati wakili Mallya alikubaliana na Jaji, ghafla anasimama wakili Nashon Nkungu.

Nkungu: Mheshimiwa Jaji nina maswali na majibu ya Mtobesya ya jana

Jaji: Umesoma wapi?

Nashon:  Wenzangu Mtobesya alikuwa ame rekodi.

Jaji: Umetoa wapi? Maana nakuona una refer kwenye simu, wala huna karatasi.

Nkungu: Alirekodi Mtobesya.

Jaji: Wewe jana uliokuwepo hapa mahakamani wakati shahidi anatoa ushahidi?

Nkungu: Hapana Mheshimiwa Jaji.

Nkungu: Basi Mheshimiwa Jaji naomba nisiendelee nishie hapo.. nikae.

Jaji: Inaonekana kuna source nyingine, maana Proceedings bado sija Certificatify, sasa huyo ana refer kwenye simu.

Jaji: Inaonekana kuna source nyingine kwenye simu zaidi yangu.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji hapana, niseme tu technology imekuwa kubwa, maana hata sisi mawakili tuna Group la WhatsApp na huwa tunashea taarifa na nyaraka humo.

Jaji: Ndiyo nimeona yeye kashika simu na ninachojua Mtobesya ameodoka  na simu yake, sasa yeye anatoa wapi au ana source nyingine.


Kibatala: Mheshimiwa Jaji naona tusifungue mambo mengime, itoshe kusema, hakuna Wakili atavunja kanuni za Mahakama wala kwenda nje ya taaluma yake, mengine ni mambo ya kibanadamu.

Jaji: Haya tuendele

Shahidi: Ukiangalia Kifungu hicho Kinatoa Exception, Pale Unapoombwa Taarifa, Paramount ni Mteja lakini Ukienda Mbele Sheria Inatoa Exception kwenye hilo suala.

Kidando:  Uliulizwa swali Kwamba mara baada ya kupokea barua kutoka kamisheni ya Uchunguzi, Kwamba Waliomba Taarifa hizo Kupitia Cyber Act, Ukasema kweli waliomba Ila ukasema Hukuona Maelezo Zaidi, labda kwa nini?

Shahidi: Hapakuwa na uwezekano wa kuomba Taarifa za ziada, vile ambavyo tumeomba ni Kwa Utaratibu wa Sheria na tulifuata Sheria

Kidando: Shahidi uliulizwa Swali kuwa Tarehe 02 July 2021 Uliombwa Taarifa, Ukajibu Tarehe 02 Julai

Kibatala: Mheshimiwa marekebisho barua Ilipokelewa tarehe 01 Julai na ikajibiwa 02 Julai

Kidando:  Ngoja nibadilishe swali, labda shahidi kwa nini ulijibu siku hiyo hiyo.

Shahidi: Ni kazi niliyo kuwa assigned siku hiyo hiyo na sababu palikuwa na volume kubwa ya kazi.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji tunaomba neno volume lisiingie.

Kidando: Hatuoni sababu, ni sawa na kuzuia shahidi kutoa ushahidi.

Jaji: Hoja yake neno volume ya kazi haku lisema mwanzo na Lisiingie.

Kidando: sawa

Kidando:  Uliulizwa swali kuhusu ku authenticate Barua hiyo, wewe ukasema barua hiyo ilikuwa imejitosheleza. Ni kwanini ulisema hivyo?

Shahidi: Sikuwa na haja ya kuona vitu vingine sababu niliona vingine vimetimia katika ile barua.

Kidando:  Kuhusu barua Iliyotoka Polisi ambayo ni Kielelezo Namba 16 kuwa palikuwa na Namba za simu pale na Fax, lakini hukuhakiki kama kweli ile narua Ilikuwa inahitaji mambo hayo.

Shahidi: Sikutaka kufanya hivyo kwa sababu barua ilikuwa inajitosheleza kutoka katika ofisi ya uchunguzi.

Shahidi: Ukiangalia Kifungu hicho Kinatoa Exception, pale unapoombwa taarifa, Paramount ni mteja lakini ukienda mbele Sheria inatoa Excepti inon kwenye hilo swala

Kidando: Uliulizwa mara baada ya kupokea barua kutoka kamisheni ya uchunguzi, kwamba aliomba taarifa hizo Kupitia Cyber Act, Ukasema Kweli Waliomba Ila ukasema hukuona maelezo zaidi, labda kwa nini?

Shahidi: Hapakuwa na uwezekano wa kuomba taarifa za ziada, vile ambavyo tumeomba ni kwa utaratibu Wa Sheria na tulifuata Sheria

Kidando: Pia ulihojiwa tarehe 02 July 2021 uliombwa taarifa, ukajibu tarehe 02 Julai

Kibatala: Mheshimiwa Marekebisho barua Ilipokelewa Tarehe 01 July na ikajibiwa 02 Julai

Kidando: Sawa labda Kwa nini ulijibu Siku hiyo hiyo.

Shahidi: Ni kazi niliyo kuwa assigned siku hiyo hiyo.

Kidando amemaliza kumhoji shahidi wao na kuiomba Mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Januari 17, 2022 itakapoendelea.

Kidando: Mheshimiwa shahidi kwa leo tulikuwa na shahidi mmoja hiyo na tunaomba ahirisho hadi Januari 17, 2022, Shahidi mwingine tuliyokuwa tunamtarajia kutoa ushahidi wake, amepata udhuru wa kuuguliwa na kwa kuwa ni Askari mstaafu bado yupo huko Handeni.

Kidando: Mheshimiwa Jaji kabla ya hujaahirisha kesi tunaomba hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mtu ambaye simu yake iliita mahakamani.

Kibando: Mtu huyu alionyesha tendo la kutokutii mwenendo wa kesi hii.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba tuende chemba tukalijadili suala hili.

Jaji: Upande wa mashtaka mnasemaje?

Kibando: Mheshimiwa Jaji ndio hoja yetu ilikuwa inaelekeza huko.

Jaji: Basi tuahirishe kwa muda, tukajadili ofisini kwangu,

Jaji: Mawakili wa utetezi na upande wa mashtaka tukutane ofisini kwangu.

Kesi imeahirishwa kwa muda kwa ajili ya jaji na mawakili kwenda kujadiliana kuhusiana na mtu mmoja anayedaiwa kurekodi Mwenendo wa kesi ndani ya ukumbi wa Mahakama wakati kesi inaendelea.

Jaji: Tuliahirisha kesi hii kwa muda kwa ajili ya kujadili suala lililojitokeza hapa mahakamani.

Jaji: Baada ya majadiliano hayo, hekima imetumika na amerudishiwa simu yake.

Jaji: Hivyo tumekubaliana pande zote mbili, kuwa mtu huyu hataruhusiwa kuingia katika ukumbi wa Mahakama kusikiliza Proceedings ya kesi hii.

Jaji: Naahirisha kesi hii hadi Januari 17, 2022, saa 3:00 asubuhi itakapoendelea na naelekeza upande wa mashtaka waje na shahidi na washtakiwa wote wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa Magereza.

Niwatakie siku njema.

High Court!!!!!!!.