Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Skendo rushwa trafiki, Masauni afunguka

Muktasari:

  • Vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kwa baadhi ya askari vinazidi kulitikisa Jeshi la Polisi nchini, huku askari wawili katika mikoa ya Iringa na Kilimanjaro wakidaiwa kukamatwa kwa nyakati tofauti kwa tuhuma hizo.

Vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kwa baadhi ya askari vinazidi kulitikisa Jeshi la Polisi nchini, huku askari wawili katika mikoa ya Iringa na Kilimanjaro wakidaiwa kukamatwa kwa nyakati tofauti kwa tuhuma hizo.

Tukio la kwanza lilitokea Ijumaa ya wiki iliyopita katika mji wa Himo wilaya ya Moshi ambapo Ofisa wa Polisi mwenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi, alikamatwa akidaiwa kupokea rushwa ya Sh20,000 ili kushughulikia dhamana ya mtuhumiwa.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikesi alikiri kukamatwa kwa ofisa huyo, lakini akakataa kuingia kwa undani akisema bado ofisi yake inaendelea na uchunguzi.

Tukio la pili ni la Askari wa usalama barabarani wa Mkoa wa Iringa, anayedaiwa kukamatwa na fedha anazodaiwa kuzikusanya kama zao la rushwa kutoka kwa madereva na wamiliki wa magari Januari 18, 2022.

Picha za tukio la kukamatwa kwa askari huyo zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii juzi jioni, zikionyesha ndani ya gari kukiwa na noti za Sh1,000, Sh2,000, Sh5,000 na Sh10,000 zilizokunjwa na nyingine askari mmoja akiwa amezishika baada ya kuzipanga.

Kufuatia tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alilieleza Mwananchi hatua za kijeshi zinaendelea kuchukuliwa.

Soma zaidi gazeti la mwananchi leo