Sugu amtumia salamu Gambo

Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi (Sugu)

Muktasari:

Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemkaribisha Tanzania aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo Jumatano Machi 1, 2023.

  

Arusha. Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemkaribisha Tanzania aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo Jumatano Machi 1, 2023.

Lema amewasili leo Jumatano Machi 1, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjarao (KIA) akitokea Canada alikokimbilia baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Lema amewasili mchana akiwa na familia yake na kupokewa na mamia ya wanachama na wafuasi wa Chadema

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Relini Arusha Sugu amesema, “kwa dogo Gambo hii ni salamu namwambia dogo kama hajajenga ajiandae kwenda kukaa kwenye geto la familia kule Ilala, lakini naamini ni mtundu mtundu”