Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sweden waadhimisha siku ya Kiswahili, Balozi Matinyi akieleza mikakati ya serikali kukieneza

Balozi Matinyi akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya siku ya kiswahili

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden ukishirikiana na jumuiya za Watanzania waishio nchini humo, umeandaa na kufanikisha sherehe za maadhimisho makubwa ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani huku serikali ikieleza mikakati ya namna ilivyojipanga kukiendeleza.

Maadhimisho haya hufanyika duniani kila mwaka ifikapo Julai  7,  na yalianza kuadhimishwa mwaka 2022  kufuatia azimio lililopitishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO)
ambapo kwa Sweden mwaka huu shughuli hiyo ilifanyikia jijini Stockholm.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mobhare Matinyi, amesema kuwa Serikali imeazimia kukieneza na kukienzi Kiswahili duniani kote huku akielezea namna kilivyosambaa.

Pia ameongeza kuwa kwa ushawishi wa Tanzania, Kiswahili sasa ni lugha ya kikazi Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

"Kwa miaka mingi lugha ya Kiswahili imekuwa kiungo cha mshikamano kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Aidha, lugha ya Kiswahili ni kichocheo cha biashara kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini - kiujumla kwenye eneo lote la nchi za Maziwa Makuu, kwani inatumiwa na wafanyabiashara wengi kwenye nchi hizi, amesema Balozi Matinyi.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa zamani wa Usawa na Jinsia nchini Sweden, Nyamko Sabuni, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) lakini aliyezaliwa Burundi na kukulia Tanzania kabla ya kuhamia Sweden.

Nyamko akitoa hotuba yake kwa Kiswahili alielezea namna lugha hiyo inavyoziunganisha nchi hizi akisema hata anapokuwa nchini Kenya kibiashara hutumia pia lugha ya Kiswahili.

Katika sherehe hizo kulikuwa na shughuli mbalimbali zinazotangaza Tanzania na utamaduni wa Mswahili kama.

Kati ya hivyo vilikuwepo vyakula, viungo, mitindo ya mavazi, sanaa za mapambo, ngoma, nyimbo, mashairi na hadithi za watoto.

Shughuli hiyo iliwakutanisha zaidi ya watu 500 ambao mbali ya Watanzania wengine walikuwa ni raia au wenye asili za nchi za Afrika Mashariki na Kati, Waswidi marafiki wa Tanzania na Mabalozi na wawakilishi wa  nchi za Botswana, China, Eritrea, India, Japan, Kenya, Misri, Nigeria, Rwanda na Zimbabwe.