Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanga yapokea fedha kujenga kituo cha damu salama

Mnganga Mkuu wa Hospitaki ya Rufaa ya Bombo, Dk Jonathan Gudenu

Muktasari:

Mkoa wa Tanga unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu salama, hivyo kujengwa kwa kituo cha damu salama kutarahisisha uboreshaji wa ukusanyaji wa damu salama katika mkoa huo kwa ajili ya wananchi wake.

Tanga. Katika kukabiliana na uhaba wa upatikanaji wa damu salama, Hospitali ya Rufaa ya Bombo imepokea Sh400 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha damu salama mkoani hapa.Hayo yameelezwa na mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Jonathan Budenu wakati wa mahojiano na gazeti la Mwananchi kuelekea mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.Dk Budenu amesema mkoa wa Tanga unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu salama na kwamba kujengwa kwa jengo hilo kutarahisisha uboreshaji wa ukusanyaji wa damu salama.“Tanga tuna uhaba wa damu salama, katika kukabiliana na changamoto hii tunajenga kituo cha damu salama na uwepo wa kituo hiki utasaidia kwa sababu hatutaagiza tena kutoka hospitali ya KCMC.“Lakini pia nitoe wito kwa Watanzania kwa ujumla kujitokeza kujitolea damu ili kuokoa maisha ya Watanzania wengine ambao wana uhitaji wa kuongezewa damu,” amesema.Budenu amesema damu haiuzwi hivyo watu wajitokeze kujitolea kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuzuia vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu.Kwa upande wao, vijana ambao wanajitolea damu kwa wagonjwa wenye uhitaji hospitalini hapo wametoa wito kwa vijana kujitokeza kuchangia damu ili kukoa maisha ya wengine.Ramadhani Msegeju, mkazi wa Mwakidila jijini hapa, amesema amekuwa akichangia damu mara kwa mara kwa lengo la kujipatia kipato kwa watu wenye uhitaji, amewatoa hofu vijana wengi ambao wamekuwa waoga kuchangia damu kwa sababu ya ukosefu wa elimu.“Mimi huwa nakuja hapa Bombo, nakaa hapa nje, kama kuna mtu anashida ya damu anataka mgonjwa wake awekewe, tunazungumza biashara. Akinipatia pesa naingia huko ndani natoa,” amebainisha Msegeju.Amesema wapo vijana wengi hufanya hivyo kwa lengo la kujipatia kipato lakini ipo haja ya Wizara ya Afya kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuchangia damu.Kwa upande wake, Mwanamvua Jumbe, mkazi wa wilaya ya Mkinga mkoani hapa, amesema wanawake ni waoga kuchangia damu kutokana kuwa na imani kwamba wanaotakiwa kufanya hivyo ni wanaume tu, hivyo elimu iongezwe ili wanawake nao waweze kujitokeza.“Mimi nilikuja hapa nikiwa mjamzito na sasa nimejifungua salama, nawashukuru wataalamu wa afya wa Bombo, wamenihudumia vizuri. Pia, niwaombe wanawake tusiogope, tujitokeze kuchangia damu kwani wakati wa kujifungua wanawake wengi hupoteza damu na wengine hutakiwa kuongezewa damu salama,” anasema  Mwanamvua.Mwezi uliopita, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alitangaza kwamba Serikali imendaa mfumo wa kadi za kieletroniki kwa wachangiaji damu na aliwataka Watanzania wajitokeze kuchangia damu  ili kuokoa maisha ya watu wanaopatwa na changamoto ya kupungukiwa damu.