Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tasaf yafikia kaya 53000 Zanzibar, kamati ya bajeti yaipongeza

Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Shedrack Mziray akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu shughuli zilizotekelezwa na mpango wa kusaidia kaya masikini upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Muktasari:

  • Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imetembelea mfuko wa Maendeleo ya jamii (Tasaf) na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi yake ya kuongeza fursa za kujiongezea kipato na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kaya masikini Tanzania Bara na Zanzibar.

Dar es Salaam. Kamati ya kudumu ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar kwa kuboresha maisha ya kaya masikini zaidi ya 53,000 visiwani Zanzibar kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Wajumbe wa kamati hiyo wamesema kwa upande wa Zanzibar maisha ya kaya hizo yamekuwa bora kwani wengi wao wamepiga hatua ya kimaendeleo ikilinganishwa na awali kabla ya kuwa katika mradi huo.

Akizungumza baada ya kufanya ziara katika ofisi za Tsaf jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Mei 2, 2025 na kupokea taarifa ya utekeleza wa mradi wa mfuko huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi, Mwanaasha Hamis Juma ameishukuru Serikali zote mbili kwa kuamua kusaidia kaya masikini kupitia mfuko huo.

"Tupo katika ziara zetu za kazi za kawaida na tunaelekea katika Bunge la Bajeti , tumekuja kwa wenzetu kuona na kupata taarifa kuhusu Tasaf na moja katika hizo taarifa za mfuko huu imesaidia kaya masikini na kuboresha miundombinu lakini kuwezesha kaya masikini... wameweza kunufuka na ni Tanzania kwa ujumla ikiwemo Zanzibar,"amesema

Nakuongeza kuwa,"Kamati ya Bajeti imekuwa ikiona maendeleo na taarifa mbalimbali kuhusu Tasaf kwa hiyo leo temukuja kuona mafanikio na changamoto lakini mengi ni mafanikio kwa maana wale walengwa wa kaya masikini wamefikiwa na mradi huu na wameweza kujinasua kiuchumi,"

Wakati mradi ukielekea kumalizika kwa kipindi cha pili Septemba, 2025, Mwanaasha ameiomba na kuishauri Serikali kuangalia namna nyinyine bora ili mradi uendelee na kuzidi kufikia kaya nyingine zaidi, huku akiitaka Tasaf kuzidi kuongeza ushirikiano, kazi kubwa wanayoifanya kwakuwa jicho kubwa liko kwao hivyo wanapaswa kukaa pamoja na Serikali kupanga mipango madhbuti ili mradi uwe endelevu na mfuko huo usonge mbele.

Mjumbe wa Kamati hiyo, Profeesa Omari Fakih Hamad amesema wamejifunza na kuona utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tasaf na kwamba changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwenye awamu ya mpango zilizopita awamu mpya unaokuja na kuendelea Serikali imekusudia kuboresha ili mpango uwe na ufanisi zaidi.

Ametoa mfano kuwa katika muongozo mpya sasa viongozi wa ngazi za chini ambao sio wa kuteuliwa na hawana mishahara kuingiza katika mpango wa Tasaf wakati awali haikuwepo huku akisisitiza kilichomfurahisha ni kushirikiana na bodi za elimu ya juu Zanzibar na Tanzania bara kuhakikisha vijana na wanafunzi kutoka kaya masikini hawapati shida katika mpango wa malipo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Shedrack Mziray amesema ni bahati kutembelewa na kamati hiyo ambapo ameifafanulia kuwa, mradi wa Tasaf umetekelezwa Tanzania bara na Zanzibar.

Amesema kwa upande wa Zanzibar mradi unaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwamba wiki ijayo wanaanza vikao vya bajeti hivyo wameona ni vizuri katika maeneo wanayoyasimamia waangalie utekelezaji na kupata taarifa fupi.

"Tumewaeleza maendeleo ya mradi na kwa upande wa Zanzibar tunashugulika na walengwa 53,000 na ujumbe mkubwa ambao tumeupeleka mradi huu umekuwa ukitekelezwa kuanzia mwaka 2021 kipindi hiki cha pili na kinakwenda kukamilika Septemba mwaka huu,"amesema

Ameongeza kuwa, "Kwahiyo kwa sasa tunawaelewesha wananchi kuhusu ruzuku ambazo tunawapatia kila mwezi pamoja na shughuli nyingi ambazo wamekuwa wakizifanya walengwa... ruzuku zitasistishwa kwa muda kuanzia Septamba mwakani. Ujumbe mkubwa Serikali iko katika maandalizi ya programu mpya ambayo tunategemea itaanza baada ya programu hii kukamilika."

Amewaomba wananchi kuwa na matumaini kuwa mradi utaendelea baada ya kukamilisha mchakato wa programu mpya na watakwenda kutambua ambao hawakufikiwa katika awamu ya sasa hivyo, watakuwa na walengwa wapya na wataendelea na taratibu kama ambavyo mradi mpya utaandaliwa.

"Kwa ujumla wajumbe wameishukuru na wamekiri kwamba programu hiyo imeleta mabadiliko makubwa kwa kaya masikini upande wa Zanzibar kwasababu kati ya kaya 53,000 zaidi ya kaya 9400 zilifanyiwa tathimini na kuonekana zimeboreka kimaisha hali zao kiuchumi zimekuwa nafuu ,hivyo walikoma kupata ruzuku Julai mwaka 2024,"amesema Mziray

Nakuongeza,"Kwahiyo wameridhishwa na utekelezaji na wameipongeza Tasaf kwa kazi nzuri wanaiyofanya kwa upande wa Zanzibar na wako tayari kuishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili nayo iweze kusimamia vizuri mradi na kuongeza bajeti katika mradi huu kwa kipindi kipya kinachokuja,"