Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA: Tumeiondoa 'task force'

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Uledi Mussa

Muktasari:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kwa sasa inatumia njia rafiki kukusanya kodi badala ya mabavu yanayoumiza wafanyabiashara.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Uledi Mussa amesema kwa sasa wanakusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara bila kutumia mabavu.


Amesema kitengo cha 'task force' kilichokuwapo huko nyuma na kutumika kukusanya kodi wamekiondoa.


Mussa amesema hayo leo Jumanne Novemba 15, 2022 katika kikao baina ya TRA na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) jijini Dar es Salaam.


"Kwa sasa tunakusanya mapato bila mabavu. Waachane kabisa kabisa na matumizi ya mabavu. Tunataka walipa kodi wajisikie vizuri kabisa. Hatuna tena Taska Force (kikosi kazi)," amesema


Mwenyekiti huyo amesema,"walipa kodi, tunawaangalia kwa macho mawili kuhakikisha wanaendelea kufanya biashara zao ili wawe walipa kodi siku zijazo."


Amesema hatua hiyo imewezesha ukusanyaji wa mapato umeongezeka akitolea mfano mapato ya Septemba yamevuka lengo badala ya kukusanya Sh6.2 trilioni wamekusanya Sh6.3 trillion.


Katika kikao hicho, wahariri wameuliza maswali mbalimbali likiwemo umuhimu wa TRA kuwaomba radhi wale wote walioumizwa na kikosi kazi hicho.


Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi, wa TRA, Richard Kayombo amesema,"kuna mengi yamefanyika nyuma ya pazia kuhakikisha yanakaa sawa. Kwa wale tuliokaa nao mmoja mmoja tumewezesha mambo kwenda sawa."


Amesema mazingira ya sasa na huko nyuma yalikuwa tofauti hivyo wanajitahidi kuweka mazingira rafiki zaidi kwa kila mmoja kufurahia anachokifanya.


Naye Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amewapongeza TRA kwa kuamua kukutana na wahariri kwani ni inaingesha hali ya kushirikiana ili kuhakikisha dhamira ya elimu kwa wananchi kuhusu kulipa kodi inafanikiwa.


"Pamoja na malalamiko yote, tunawapongeza sana, kwa sasa hatujaona makufuri yakifungwa kwa wafanyabiashara, hili ni jambo zuri," amesema


Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa TEF,  Bakari Machumu amepongeza jitihada zinazofanywa za kuweka mazingira mazuri ya kulipa kodi hilo linatia moyo.


Machumu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) amesema, kila mmoja akiwa na uelewa wa pamoja na shirikishi hata mapato yataongezeka.