Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tume haki jinai yaanza uchambuzi wa maoni

Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Jaji Mstaafu, Othman Chande akizungumza na waandishi wa habari  leo Mei 2, 2023 jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wao na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja na wakuu wa taasisi za kimataifa kumalizika. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Tume ya kuboresha mifumo na taasisi za haki jinai nchini imeanza kufanyia uchambuzi maoni iliyokusanya.

Dar es Salaam. Baada ya miezi mitatu ya kukusanya maoni ya wadau, hatimaye Tume ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai nchini, imeanza uchambuzi ili kutoa rasimu ya awali ya mapendekezo.

Tume hiyo iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Januari mwaka huu na kuanza kazi Februari 1, 2023, imesema imani ya wananchi juu ya taasisi hizo ndiyo shabaha yake.

Kauli hiyo, imetolewa jijini Dar es Salaam leo Jumanne ya Mei 2, 2023 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Mohammed Othman Chande, alipozungumza na Waandishi wa habari baada ya kikao na mabalozi na Wakuu wa taasisi za kimataifa.

Kazi hiyo ya uchambuzi wa maoni yaliyokusanywa, amesema inatarajiwa kufanyika kwa mwezi mmoja kisha itatolewa rasimu ya awali ya mapendekezo.

"Kazi ya uchambuzi tutaifanya kwa siku 30 kisha tutatoa rasimu ya awali ya mapendekezo, hiyo itahusisha yanayopaswa kutekelezwa haraka, ya muda wa kati na mrefu," amesema.

Kwa mujibu wa Jaji Chande, shauku ya wananchi ni kuwa na imani na taasisi za haki jinai na kinachofanywa na tume hiyo kunalenga kufanikisha hilo.

"Kuna shauku kubwa ya wananchi kuona mageuzi katika taasisi za haki jinai na tunatarajia mapendekezo yetu yafanikishe hilo," ameeleza.

Katika kipindi hicho cha miezi mitatu kwa mujibu wa Chande, takriban wananchi 10,000 wamesikilizwa, katika mikutano 25 ya hadhara, iliyofanywa katika Wilaya 53 na Mikoa 25.

Kuhusu kikao hicho na mabalozi, amesema kimelenga kuwapa taarifa ya kinachofanywa na tume kwa kuwa nao ni sehemu ya wadau.

"Taasisi za kimataifa wakati mwingine zinafanya kazi na taasisi za haki jinai, tumeona tuwafahamishe kwa kuwa nao ni wadau. Pia tunawakaribisha watoe mapendekezo yao kwa sababu huu sio mwisho wa kupokea maoni," ameeleza.