Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tumieni vifaa kuzuia madhara ya kemikali

Baadhi ya madereva wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa katika  mafunzo maalum kuhusu usafirishaji salama wa kemikali.

Muktasari:

Wasimamizi wa kemikali katika maneo ya migodini, viwandani, wauzaji na madereva wanayoisafirisha wametakiwa kutumia vifaa kinga wakati wa shuguli zao kuepuka madhara yake.

Mwanza. Wasimamizi wa kemikali katika maneo ya migodini, viwandani, wauzaji na madereva wanayoisafirisha wametakiwa kutumia vifaa kinga wakati wa shuguli zao kuepuka madhara yake.

Akifunga mafunzo ya siku mbili ya usimamizi salama wa kemikali yaliyojumuisha mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana, Katibu Tawala Msaidizi upande wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Patrick Karangwa alitaja vifaa hivyo ni barakoa (mask) na vikinga mkono (groves).

Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo alisema mikoa ya Kanda ya Ziwa inaongoza kwa matumizi ya kemikali kutokana na shuguli za uchimbaji madini huku akiutaja Mkoa wa Mwanza kuongoza kuwa na wafanyabiashara wengi wa kemikali na kuwataka watumie matumizi salama ya bidhaa hiyo.

“Tunaamini kupitia elimu tuliyoitoa kwa siku mbili kuna kitu ambacho washiriki wameongeza na lengo waweze kufikia kile ambacho tunatarajia cha matumizi salama ya kemikali kwenye hatua zote iwe kuiuza, kuitumia, kuisafirisha na mwisho tuendelee kutumia kemikali salama sisi pamoja na jamii yetu lakini pia tuache mazingira yakiwa salama leo, kesho pamoja na vizazi vijavyo,”amesema Daniel

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, yamejumuisha Maofisa Afya, madereva wanaosafirisha kemikali, Wasimamizi wa kemikali pamoja na wahandisi lengo likiwa ni kuwapa uwezo wa kusimamia kemikali zilizopo kwenye maeneo yao, kulinda afya za wafanyakazi, jamii nzima na kulinda mazingira.

Mmoja wa madreva wa magari ya masafa marefu yanayosafirisha kemikali mkoani Kagera, Habibu Amiri amewashauri  madereva kuacha tabia ya kutumia kilevi wakiwa kazini  ili kuepuka ajali.

“Dawa tunazosafirisha kwenye magari yetu yanahitaji umakini kwa sababu yana madhara kiafya na kimazingira yasiposhughulikiwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu ikiwemo kuvaa mavazi maalum na kuendesha kwa tahadhari kuepuka ajali,” amesema

Rose Dominic, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo aliishukuru Serikali kwa kutoa elimu ya matumizi na udhibiti wa kemikali katika matumizi ya kiuchumi akisema inalinda siyo tu afya, bali pia mazingira.