Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchakavu choo cha mwaka 62 chawaibua wadau

Muonekano wa vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wereni ambavyo viimejengwa tangu mwaka 1962.

Muktasari:

  • Uchakavu wa matundu ya vyoo Shule ya Msingi Wereni, Kijiji cha Umbwe Sinde, wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro iliyojengwa miaka 62 iliyopita, wamefanya waliowahi kusoma hapo, kumalizia ujenzi wa choo kipya cha kisasa.

Moshi. Uchakavu wa matundu ya vyoo Shule ya Msingi Wereni, Kijiji cha Umbwe Sinde, wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro iliyojengwa miaka 62 iliyopita, wamefanya waliowahi kusoma hapo, kumalizia ujenzi wa choo kipya cha kisasa.

Shule hiyo ambayo ina jumla ya wanafunzi 224 wamekuwa wakitumia choo hicho chenye matundu 20 licha ya kwamba ni chakavu hali ambayo inahatarisha usalama wa wanafunzi hao.

Hata hivyo, ujenzi huo wa choo kipya ulikwama ulipofikia hatua ya kupaua, kutokana na kile kilichoelezwa “ukata wa kifedha” na hivyo kuwalazimu wanafunzi hao kuendelea na matumizi ya choo hicho hatarishi.

Akizungumza Mwananchi Digital, mmoja wa waliojitolea kumalizia ujenzi huo, Deo Mushi amesema baada ya kuona wanafunzi wako kwenye hatari kutokana na ubovu wa choo hicho aliamua kutoa mabati hayo ili kukamilisha ujenzi wake.

"...hiki choo ni kile cha miaka ya 60 ambacho walitumia wazazi wetu...kina hali mbaya, nikaona nilazima tushirikiane na Walimu na wadau wengine kuhakikisha hiki choo kinakuwa katika ubora wake, kwa kweli kazi imeshafanyika kilichobaki ni kuweka lenta na bati," amesema na kuongeza;

"Na kwa kuwa mimi ni mdau wa maendeleo kwenye kata yangu hii, naangalia pale ambapo naweza kushirikiana na wenzangu kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri, hivyo tumeleta bati 40 ili angalau watoto wapate mahali pazuri pakujisitiri.”

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Francis Msacky amesema choo hicho kimejengwa kwa muda mrefu bila kumalizika kutokana na changamoto ya upatikanaji wa fedha.

"Tulikuwa na uhitaji mkubwa sana wa fedha, mabati haya yatatusaidia kwa kiasi kikubwa kumalizia ujenzi wa choo chetu hiki ambacho kwa kweli kimejengwa kwa muda mrefu bila kukamilika,” amesema mwalimu huyo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, John Shamali amesema: "Ni muda mrefu tumejaribu kuomba wananchi wa kijiji hiki ili wachangie ujenzi wa choo hiki, hata walipochanga, hatukuweza kupata kiasi cha kutosha.”

Jonas Mallya, ni mwanafunzi wa darasa la tano shuleni hapo, yeye anasema kwa muda muda mrefu amekuwa akiogopa kutukitumia choo cha zamani kwa kuhofia usalama wake, hivyo kukamilika kwa ujenzo wa choo kipya ni habari njema siyo tu kwake bali kwa wanafunzi wenzake pia.