Ulinzi waimarishwa mipakani mwa Kenya
Muktasari:
Akizungumza ofisini kwake juzi, Kamanda wa kanda hiyo, Henry Mwaibambe alisema kuna uwezekano wa raia kutoka Kenya kuingia nchini kinyemela wakikimbia vurugu zinazotokana na uchaguzi huo.
Tarime. Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya imesema inaimarisha ulinzi kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania, kutokana na uchaguzi wa marudio unaoendelea nchini humo.
Akizungumza ofisini kwake juzi, Kamanda wa kanda hiyo, Henry Mwaibambe alisema kuna uwezekano wa raia kutoka Kenya kuingia nchini kinyemela wakikimbia vurugu zinazotokana na uchaguzi huo.
“Tumeamua kuimarisha ulinzi maeneo hayo baada ya uchaguzi wa awali, Wakenya wengi waliingia nchini kinyume na utaratibu,” alisema.
Kamanda Mwaibambe alisema hayo wakati akishiriki usafi wa mazingira unaofanyika kila mwisho wa mwezi. Alisema licha ya kulinda raia na mali zao, polisi wanashiriki shughuli za jamii. (Waitara Meng’anyi)