Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UN-ICTR yamaliza kazi nchini

Muktasari:

  • Yaiachia kibarua Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (MICT)

Arusha. Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) imefunga shughuli zake nchini huku ikiiachia kazi Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (MICT) cha upatikanaji, ukamataji na usikilizwaji wa kesi ya watuhumiwa tisa wa mauaji.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi ujenzi wa bustani wenye mnara wa kumbukumbu na elimu ya shughuli za mahakama hiyo nchini, Rais wa UN-ICTR,  Vagn Joensen alisema wametekeleza majukumu yao kwa amani miaka yote hadi sasa walipofunga mahakama hiyo bila bughudha.

“Tunashukuru Serikali ya Tanzania na Arusha yake kwani tumekaa kwa muda mrefu wa miaka 21 sasa na kufanikisha shughuli hii, hadi leo tunafunga,” alisema Joensen  na kuongeza:

“Ila bado washukiwa tisa hawajakamatwa lakini kutokana na muda wetu kuisha tunaiachia MICT iliyoko hapa Arusha ishughulike nao na naamini mtawapa ushirikiano mliotupa.”

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fadhili Nkulu alisema kumbukumbu hiyo iliyoachwa na UN- ICTR itakuwa  sehemu ya kituo cha elimu kwa watu wote kujifunza juu ya mauaji ya kimbari na shughuli za mahakama hiyo.

“Tuseme tu ahsante kwa wafanyakazi kuona umuhimu wa kuacha kumbukumbu hii ya bustani itakayokuwa na mnara wa UN-ICTR na pia mnara wa Mwalimu Nyerere (Julius) ambao mbali na kuwa sehemu ya burudani kwa wakazi wa Arusha na michezo ya watoto pia itakuwa kama sehemu ya kutoa elimu na tunaahidi kuitunza na kuienzi,” alisema.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Iddi Juma akipokea bustani hiyo alisema itakuwa moja ya sehemu za wazi za wakazi wa Arusha kupumzika baada ya kazi.

Mahakama hiyo iliyokuwa na wafanyakazi zaidi ya 1,500 kutoka nchi 100 duniani wakiwamo majaji na mahakimu ilifanikiwa kukamata watuhumiwa 83 wengi wao wakiwa viongozi wa kisiasa, kijeshi na kidini waliokuwa wakiwatafuta kwa tuhuma za kusababisha mauaji hayo.

Hata hivyo, washukiwa tisa hawajakamatwa na shughuli hiyo sasa itafanywa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa ICTR, Danford Mpumiliwa, mahakama hiyo iliundwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lengo likiwa ni  kuhakikisha watu wote waliokamatwa na kuhukumiwa kutumikia vifungo vyao katika magereza sehemu mbalimbali duniani.