Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UN yataka kasi utokomezaji umasikini

Muktasari:

  • Wakati utekelezaji wa maendeleo endelevu ukiendelea kufanywa na nchi mbalimbali imeelezwa kuwa utokomezaji umasikini bado uko chini

Dar es Salaam. Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Zlatan Milisic amesema bado kuna kusuasua katika utekelezaji wa baadhi ya malengo endelevu nchini na duniani kwa ujumla ikiwemo lengo namba moja la kutokomeza umasikini kwa watu.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumzia na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 78 ya Umoja wa Mataifa yanayotarajiwa kufanyika kesho Oktoba 24, 2023 jijini hapa huku yakibebwa na kaulimbiu isemayo ‘Wekeza leo kwa ajili ya kesho kwa kuinua vijana wa Kitanzania’.

Hafla hiyo itahusisha pia kupandisha bendera ya Tanzania, huku ikenda sambamba na gwaride la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambavyo vyote kwa pamoja vitahamasisha vijana kujiajiri ili waweze kuchangia katika maendeleo ya nchi.

Akizungumza Milisic amesema katika Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa lililofanyika jijini New York nchini Marekani Julai mwaka huu, Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba ameelezea namna Tanzania inavyofanyia kazi malengo endelevu huku akieleza kuwa kama nchi inafanya vizuri katika utekelezaji wa lengo namna 2 hadi 8.

Malengo hayo ni yale yanayohusu kutokomeza njaa, afya, elimu bora, usawa wa kijinsia, majisafi na usalama wa mazingira, nishati safi na nafuu, kazi zenye staha na ukuaji wa uchumi.

“Lakini utekelezaji upo kwa kiasi kidogo katika lengo namba moja ambalo ni kutokomeza umasikini. Miongoni mwa watanzania bado wana changamoto ya umasikini jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi na hii si Tanzania pekee bali nchi zinazoendelea zinapaswa kuongeza nguvu katika kukabiliana nayo,” amesema Milisic.




Amesema maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika katika sekta ya kilimo yanaweza kuchangia kwa kiasi kufanikisha utekelezaji wa lengo hilo kwani kilimo kinagusa takribani robo tatu ya Watanzania.

Pia, amesema kuwapo kwa ongezeko la bajeti ya kilimo mwaka hadi mwaka ni ishara kuwa maboresho zaidi yanaendelea kufanyika na kugusa idadi kubwa ya watu.

Bajeti ya Wizara ya Kilimo imekuwa ikipaa kwa miaka mitatu mfululizo ambapo kwa mwaka 2022/23 imepanda kutoka Sh751.12 bilioni hadi kufikia Sh970.78 bilioni mwaka 2023/24 sawa na ongezeko la asilimia 29.24.

Hili pia linasemwa wakati ambao serikali inaendelea kutekeleza kuboresha hali za maisha ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri kupitia programu mbalimbali ikiwemo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Kupitia mpango huo, hadi Desemba 2022, kaya 1,371,038 zenye wanufaika 6,596,820 zilinufaika na mpango huo ikilinganishwa na kaya 1,279,433 zilizokuwa na wanufaika 6,396,620 katika kipindi kama hicho mwaka 2021.


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda amesema malengo ya maendeleo endelevu ni muhimu na yapo mafanikio ambayo yamepatikana kutokana na jitihada za serikali lakini bado kuna kipande cha kufanya kwa ajili ya kufikia malengo yaliyowekwa.

“Mpango wa maendeleo unaotekelezwa sasa unahakikisha kasi na nchi mbalimbali ziliathiriwa na changamoto zilizpoikumba dunia ikiwemo ugonjwa wa Virusi vya Korona, Tanzania iliathirika kwa kiasi hivyo tuna imani tutafikia malengo mengi kati ya yale 17 yaliyowekwa,” amesema Kaganda.


Amesema katika utekelezaji wa malengo hayo, Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza vijana wa Kitanzania ikiwemo kwa kuwapatia Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kuendeleza miradi yao 85 katika sekta ya kilimo voiwanda na biashara kupitia mfuko wa kuwezesha vijana.

Pia vijana wameendelea kuwekezeshwa katika ya kilimo kupitia Mpango wa Jenga Kesho iliyobora (BBT) ambayo inalenga kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo kwa kuwapatia ujuzi na mitaji.