Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unyanyasaji dhidi ya wanawake waripotiwa Pakistan

Muktasari:

  • Imeelezwa kuwa unyanyasaji dhidi ya wanawake nchini Pakistan ni tatizo linaloota mizizi katika kaya mbalimbali na sasa limeanza kuibua hofu miongoni mwa jamii.

Imeelezwa kuwa unyanyasaji dhidi ya wanawake nchini Pakistan ni tatizo linaloota mizizi katika kaya mbalimbali na sasa limeanza kuibua hofu miongoni mwa jamii.

Wanaharakati nchi humo wanaeleza kuwa baadhi ya wanaume wanadhibiti wanawake kwa kuwanyanyasa  hadharani, kuwabaka au kuuawa na wanaume wanafanya uhalifu huo bila hofu ya kuadhibiwa au kushtakiwa kama alivyoleza Mehmil Khalid katika gazeti la Dunyanews.

Pakistan imepitisha  sheria za kudhibiti unyanyasaji dhidi ya wanawake lakini sheria hiyo inatekelezwa kwa kiwango cha chini jambo linalochangia kesi kutofikia mwisho na ni kama inatoa uhalali kwa wanaume kuendelea kuzingatia kutojali na kuwadhulumu wanawake na kukiuka sheria.

Utafiti wa  Wizara ya Haki za Kibinadamu ya Pakistan iliyotaja idadi ya watu na afya wa nchi hiyo (2017-2018), unaeleza  karibu asilimia 28 ya wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15 na 29 wamefanyiwa ukatili.

Unaeleza kuwa baadhi ya kesi zilizosajiliwa polisi zina takwimu zisizo sahihi ambazo hazifafanui uhalifu wa kikatili uliofanywa dhidi ya wanawake nchini Pakistan.

Shirika la Haki za Binadamu katika ripoti yake ya mwaka ya dunia 2022,  ilitaja madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki dhidi ya wanawake pamoja na watoto nchini Pakistan, ambayo inashikilia nafasi ya 167 kati ya nchi 170.

"Unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana, ikiwa ni pamoja na ubakaji, mauaji, mashambulizi ya tindikali, unyanyasaji wa nyumbani na ndoa za kulazimishwa zimeenea kote Pakistan. Watetezi wa haki za binadamu wanakadiria kuwa takriban wanawake 1,000 wanauawa katika kile kinachoitwa mauaji ya heshima kila mwaka,” imeeleza ripoti ya HRW.

Kwa mujibu wa Dunyanews, mwanaharakati mashuhuri wa haki za wanawake, Farzana Bari amesema sababu ya kukithiri kwa kesi za ukatili dhidi ya wanawake nchini Pakistan ni kutokana na kutokuwapo kwa umakini kwa serikali kuzindua utekelezaji madhubuti wa sheria na kuelimisha, kuwawezesha wanawake kukandamiza mitazamo ya kibaguzi dhidi yao.

"Hakuna serikali iliyowahi kujaribu kukomesha mawazo haya. Inaweza kufanyika kwa kuelimisha wanawake katika maeneo ya vijijini, kuwawezesha kiuchumi na kuinua uwakilishi wao katika Bunge,” aliongeza.

Kutokana na kutotekelezwa kwa sheria na kuwaadhibu wahalifu, viwango vya uhalifu vinaongezeka na vinaweza kuzuiwa iwapo tu sheria zitatumika katika kushughulikia masuala hayo, wamesema wachambuzi hao waliotaka kuwepo kwa hitaji la haraka la kudhibiti ukatili dhidi ya wanawake.

Walipendekeza kuwa sehemu zote za jamii zinapaswa kuwa na jukumu sawa katika kutokomeza kabisa kutoka maeneo ya vijijini. Inapaswa kuchukuliwa kama somo kubwa ambalo linafanya maisha ya wanawake kuwa hatarini.

Wanawake wanapaswa kujengewa uwezo dhidi ya vitendo hivyo ili waweze kuwa walinzi wao wenyewe, wachambuzi walisema, wakitaka kuwepo kwa mpango kabambe wa marekebisho ya pamoja unaojumuisha hatua za kinga na mageuzi mbalimbali ya kusaidia katika kuondoa tishio hili katika jamii.

Mwaka jana, Pakistan iliorodheshwa katika nafasi ya 153 kwenye faharasa ya pengo la jinsia ulimwenguni kwa kuzingatia hali ya kutisha na usumbufu ambao wanawake wanaupata.