Uswisi, Tanzania: Karne ya historia ya pamoja

Kutoka kushoto ni Senorina Lukwachala, Joyce Seki, Eutropia Nduye, Franciscan Masista wa Charity, Mbingu, Tanzania Picha na Magali Rochat.

Muktasari:

  • Tanzania ulianza mwaka 1921, wakati ndugu Wakapuchini wa Kifransisko na Masista wa Baldegg walipoanzisha shughuli zao za kidini katika Wilaya ya Kilombero, kilomita 400 kutoka jijini Dar es Salaam, Kusini-Magharibi mwa nchi.

Tanzania ulianza mwaka 1921, wakati ndugu Wakapuchini wa Kifransisko na Masista wa Baldegg walipoanzisha shughuli zao za kidini katika Wilaya ya Kilombero, kilomita 400 kutoka jijini Dar es Salaam, Kusini-Magharibi mwa nchi.

Wamisionari walianzisha hospitali na shule kadhaa, ikiwa ni pamoja na Hospitali ya St Francis huko Ifakara, ambayo sasa inahudumia idadi ya watu wapatao milioni moja.

Uswisi imeendelea kuleta mabadiliko chanya katika kanda tangu wakati huo. Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC), ambalo ni idara ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje (FDFA) ya Uswisi, linasaidia miradi kadhaa nchini na mwaka huu linaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.

Masista wa Baldegg pia walianzisha usharika wa Masista wa Kifransisko wa Upendo Mahenge (Franciscan Sisters of Charity of Mahenge) ambao wanaendeleza kazi ambayo wamisionari wa Uswisi walianzisha nchini miaka 100 iliyopita.

Anasema, “Masista wa Baldegg ni sawa na mama zetu wa damu,” alisema Sista Joyce Seki, huku akiachia tabasamu kubwa.

Katika jengo la Laverna lililopo eneo la Mbingu, umbali wa masaa kadhaa kwa usafiri wa gari kutoka Ifakara, tuliisikiliza hadithi ya Sista Joyce kwa shida kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha juu ya paa la bati. Kwa sauti ya kuyumbayumba, alieleza kuwa hajui umri wake halisi.

“Nilitajiwa miaka mitatu tofauti nilipozaliwa na nilichagua mwaka ule niliouona unanifaa zaidi ambao ni 1943.” Umri wa Joyce ni sawa na Usharika wa Dayosisi ya Masista wa Kifransisko wa Upendo, ulioanzishwa na Masista wa Baldegg mwaka 1944.

Alama iliyoachwa na Uswisi ni vigumu kusahaulika ikiwamo kuta zilizopambwa kwa picha kadhaa za viongozi wakuu wa usharika kwa miongo kadhaa. Joyce, ambaye alikuwa kiongozi mkuu kwa miaka 15, alituonyesha moja ya picha ya mwalimu wake wa kwanza, Sista Christophora Kunzli, kiongozi mkuu wa usharika kuanzia mwaka 1953 hadi 1970. "Nilipofika ngazi ya elimu ya sekondari, alikuwa mwalimu wetu baada ya shule kufungwa.

Hakuwahi kukosa hata kipindi kimoja darasani, bila kujali idadi yetu, aidha tulikuwa wawili au kumi. Alikuwa akifundisha kwa mtindo ule ule. Aliwahi kusema, “Maisha yana maana ikiwa tu unawajali wengine,” Sijawahi kusahau kanuni hii na nimeiishi kwa kipindi chote hicho.

Maadili ya Uswisi

Masista wa Baldegg walijijen-gea heshima kubwa katika mkoa huo kama wanawake wa vitendo zaidi. “Tulijifunza si tu kwa nadharia bali kwa vitendo,” anaeleza Sista Senorina Lukwachala, ambaye alikuwa msaidizi kiongozi mkuu wa usharika kwa miaka tisa iliyopita.

Moja ya alama kubwa za mafanikio ya Hospitali ya St Francis iliyopo Ifakara, iliyoanzishwa na ndugu Wakapuchini wa Kifran-sisko mwaka 1927 na kuendeshwa na Masista wa Baldegg hadi mwaka 1976, leo inahudumia wakazi milioni moja wa Mkoa wa Morogoro.

Sista Senorina aliletwa katika ulimwengu huu miaka 50 iliyopita na nesi wa Kiswisi katika hospi-tali hii. “Nilipokuwa mdogo hapo Ifakara kila mtu alikuwa akiwa-jua Masista hawa wa Uswisi, kila uendapo ilikuwa lazima ungekutana na shule na zahanati zao.

Kumbukumbu ya Sista Maria-Paula bado inaenziwa katika Kituo cha Ukoma cha Nazareth kilichopo Ifakara ambacho ni maarufu kwa jina la “Paula Cen-ter.” Mfano mwingine ni Sista Prudencia, aliyepewa jina la utani “Dada Kasumuni” kwa sababu alikuwa akiwatoza wagonjwa gharama ya matibabu kwa senti 50 ya shilingi ya Tanzania (thumuni) katika dawati la mapokezi la Hos-pitali ya St Francis.

Masista hawa watatu ambao ni mfano wa kuigwa walimpa saba-bu Sista Eutropia Nduye, kiongozi mkuu wa usharika tangu mwaka 2012, kujiunga na usharika huo. “Nilivutiwa kujiunga nao baa-da ya kazi nzuri ambayo Masista wa Baldegg walikuwa wakiifanya kwa mkoa mzima.” Alisisitiza.

Sista Joyce Seki, Kiongozi Mkuu (2006-2012), wa Franciscan Sisters of Charity, Mbingu, Tanzania akionyesha picha ya Mwalimu wake Christophora Kuzli, Sista wa Baldegg 1953-1970. Picha na Magali Rochat.

Kwa sasa wanachofanya ni kufuata tu nyayo za ‘mama’ zao. “Walitufundisha sisi, Masista wao wa Kiafrika kila kitu. Walitufundisha wanachojua, walituhimiza kwenda shule, kupata elimu, kuwa wasomi, na walipoona tuko tayari, waliondoka.

”Ingawa wapo Wamision-ari kadhaa wa Uswisi waliooa waliopumzishwa kwenye nyumba zao za milele Tanzania, Masis-ta wa Uswisi walioishi Ifakara waliondoka nchini miaka mitatu iliyopita ili kutumia siku zao za mwisho katika jimbo la Lucerne. “Walitufundisha ujuzi wao wote na leo tunaweza kusema kwamba tunaendelea na kazi waliyoianza.”

Urithi endelevu

Usharika wa Masista wa Kifransisko wa Upendo umekuwa ni taasisi huru ya utoaji wa misaada tangu 1971. Usharika huo una idadi ya Masista wapatao 300 ambao wanafanya kazi ya hisani iliyoanzishwa na dada zao walio-watangulia.

Wakitekeleza shughuli zao katika kijiji cha Mbingu tangu miaka ya 1990, Masista hao wa Kitanzania wanamiliki sehemu ya ardhi yenye ukubwa wa hekta 3,000 ambapo kupitia msaada wa fedha kutoka kwa Taasisi ya Masista wa Baldegg, wamejenga zahanati, kituo cha watoto yatima, kituo cha mafunzo na shule ya sekondari ya wasichana ambayo inachukua hadi wanafunzi 300.

Zaidi ya watu 20,000 katika mkoa huo, sasa wananufaika na huduma zao. Na hawana nia ya kuishia hapo. Shule ya wavulana tayari ipo katika mipango yao. “Hakuna kinachoweza kuzuia kazi ambayo Masista wa Baldegg waliianza, labda kama nchi hii haitakuwepo tena,” alisema Sista Senorina.

Hata hivyo bado changamo-to ni nyingi. Kijiji cha Mbingu bado hakijaunganishwa kwenye gridi ya Taifa. Katika jitihada za kuhakikisha jamii inafikiwa na huduma ya umeme, mwaka 2008, Masista wa Baldegg walinunua kituo kidogo cha kufua umeme wa maji, chenye uwezo wa kuzalisha kW 850, ambacho kiko kilomita 14 kutoka katika jengo la Laverna.

Hata hivyo, kwa sababu eneo hilo hukabiliwa na mafuriko wakati wa mvua, kituo hicho cha umeme kinahitaji matengenezo ya kutosha kutokana na athari za uharibifu na uchakavu, bila ya kusahau kuwa nyumba ya Masista hao imekosa umeme kwa zaidi ya miaka mitatu.

“Tulikuwa na jenereta kwa ajili ya kutoa huduma muhimu, lakini ilikuwa ghali sana ikatubidi tusitishe baadhi ya shughuli zetu, ndugu zetu wa Uswisi (Masista wa Uswisi) hawakuwa na uwezo tena wa kutusaidia kifedha, hivyo tulilazimika kutafuta ufadhili sehemu nyingine.

”Kutokana na uzoefu huo wilay-ani Kilombero na ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, Uswisi kupitia ubalozi wake nchini, iliamua kuchangia kiasi cha CHF 112,000 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha kufua umeme wa maji.

Ukitekelezwa na kuratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Uswisi la Solidarmed, mradi huo ulikamilika Januari 2021.

“Tunashukuru kwa msaada huu. Watoto wa kituo cha watoto yatima wanapata umeme nyakati za jioni tena, tumeweza kuendelea na huduma katika zahanati na hivyo tunaendelea kutoa huduma kwa jamii ambayo Masista wa Baldegg walianza nayo karibu karne moja iliyopita,” alieleza Sista Joyce Seki, akionekana kuguswa zaidi, huku akiongeza kuwa, “Ikiwa kuna jambo moja tunalopaswa kujifunza kuhusu Waswisi, ni kwamba wanapoanzisha jambo, wanalifanya hadi mwisho

 #SDC40TZ  #SwissEmbassyTZ