Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utafiti: Imani ya wananchi kwa Mahakama imeongezeka

Muktasari:

  • Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini (REPOA) umeonyesha kuongezeka kwa imanbai ya wananchi kwa mhimili wa Mahakama kutoka asilimia 78 mwaka 2019 hadi asilimia 88 mwaka 2023.

Dar es Salaam. Wananchi wengi wameeleza kuendelea kuiamini na kuridhishwa na huduma za Mahakama ya Tanzania, kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini (REPOA) mwaka 2023.

Taasisi hiyo inayojishughulisha na utafiti katika uchumi, jamii na maendeleo na Sera

Matokeo ya ufafiti huo yametangazwa leo Jumanne Julai 11, 2023, na kukabidhiwa kwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Wilbert Chuma, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke.

Akitangaza matokeo ya utafiti huo mkurugenzi wa utafiti na mafunzo wa Repoa, Dk Lucas Katela amesema kwamba kuwa lengo la utafiti huo ni kuboresha shughuli za kimahakama ziwe kama kibiashara na kuweza kufikia viwango vya kimataifa.

“Utafiti huu unaonesha tulikofikia na kupendekeza nini kifanyike kuboresha zaidi,” amesema Dk. Katela.

Amebainisha kuwa katika utafiti huo waliwahoji watu wengi hususani walioko mahakamani (wateja) na wasio wateja wa mahakama (wasio na kesi mahakamni) wanaume kwa wanawake, watumishi wa mahakama katika ngazi mbalimbali za mahakama kuanzia Mahakama za Mwanzo mpaka Mahakama ya Rufani.

Kwa mujibu wa Dk Katela ilibainika kwamba wanaume wengi ndio wako mahakamani kwa asilimia 69 wakati wanawake wakiwa ni asilimia 31 tu na kwamba hali hiyo inaweza kuonesha kuwa ama ndio wanafanya makosa sana au wanadai haki zao sana.

Katela amesema kwa ujumla kiwango cha wanachi kuridhika na mahakama kimeongezeka kutoka kufikia asilimia 88 kutoka asilimia 78 kwa mwaka 2019.

Pia amesema kuwa wananchi wengi wanajua ni kwa nini wanakwenda mahakamani kuwa ni kwa ajili ya kupata haki yao jambo ambalo amesema ni muhimu.

Hata hivyo, amesema kwa upande wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi asilimia 33 wameelezea kutokuridhishwa.

Amebainsiha maeneo au vingele mbalimbali vilivyohusijka katika utafiti huo ambavyo vyote katika ujumla wake wananchi wameoneshwa kuridhishwa.

Ubora wa huduma

Kwa upande wa ubora wa huduma kiwango cha wananchi kuridhika kimeongezeka kufikia asilimia 62 kulinganisha na asilimia 55 mwaka 2019.

Huduma, uwezo na maadili ya watumishi wa Mahakama.

Asilimia 94 wameelezea kuridhishwa na namna walivyohudumiwa na watumishi wa mahakama kulinganisha na asilimia 89 mwaka 2019, huku asilimia 92 wakielezea kuridhika na uwezo wa watumishi wa mahakama kulinganisha na asilimia 82 kwa mwaka 2019.

Kwa upande wa maadili ya kazi kwa watumishi wa umma, asilimia 92 ya wananchi wameelezea kuridhishwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 kulinganisha na mwaka utafiti uliopita wa mwaka 2019

Muda wa kupata huduma

Katika eneo hilo, utafiti umeonyesha kiwango cha uharaka wa kupata huduma kimeongezeka mpakam asilimia 74 kutoka asilimia 71 kwa utafiti wa mwaka 2019.

Matarajio

Asilimia 50 wameeleza kuwa waliukuta zaidi ya walichotegemea yaani waliukuta hali nzuri kuliko walivyokuwa wanadhani, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.

Mahakama za Watoto

Asilimia 67 wameelezea kuridhishwa na usiri wa taarifa za kesi za watoro kulinganisha na asilimia 57, huku asilimia 63 wakielezea kuridhishwa na usikilizwaji kwa wakati wa kesi hizo kulinganisha na asilimia 52 mwaka 2019.

Mazingira ya kazi kwa watumishi

Maneo mengine yaliyohusishwa kwenye utafiti huo ni mazingira ya kazi kwa watumishi wa mahakama ambapo watumishi 76 waemeelezea kuridhishwa na mazingira ya kazi kulinghanisha na aslimia 60, mwaka 2019,

Asilimia 92 wameleezea kuridhishwa kuipata kwa wakati lakini wengi wakielezea kutokuridhishwa na kiwango cha mishahara wanayolipwa, huku asilimia 72 ya watumishi wa mahakama wameelezea kuridhishwa kulinganisha na asilimia 54 utafiti uliopita.

Hata hivyo bado wananchi wengi hawana ufahamu wa kuwepo kwa mahakama inayotembea kwani asimilia 27 tu ndio wameeleza kufahamu kuwepo kwayo ikiwa ni ongezeko la asilimia moja tu kutoka mwaka 2019 ambapo walikuwa asilimia 26.

Mapendekezo

Kutokana na utafiti huo Repoa imependekeza mahakama iendelee kupanua zaidi miundombinu kwani kutokana na kufanyika na licha ya upanuzi huo kufanyika mahitaji nayo yamezidi kuwa mengi, huku ikipendekeza kuongeza matumizi ya mahakama inayotembea kama suluhisho la ndani.

Pia imependekeza kuongeza muda wa kumalisha mashauri tangu yanapofunguliwa, kufanya ukaguzi hasa kwa mahakama za chini kuhusu maadili, kutoa elimu kwa watumishi kuhusu vigezo vya kupandishwa madaraja.


Vilevile imependekeza kuongeza elimu kwa umma kuhusu njia za mawasiliano, hususan matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), na kuwepo kwa vituo vya mahakama vya kupokelea malalamiko kuhusiana na masuala mbalimbali.

Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Chuma amesema kuwa mahakama imekuwa ikifanya maboresho ili kutoa huduma bora kwa mwananchi.

“Aidha, katika kujipima kuhusu kiwango cha kuridhika kwa wananchi kuhusu huduma zitolewazo na Mahakama, Mahakama imekuwa ikifanya utafiti kupitia mtafiti huru (consultant) REPOA.

“Lengo la utafiti huo ni kupata maoni ya wananchi juu ya kuridhika kwao na huduma zinazotolewa na mahakama ili kubaini maeneo yenye mafanikio na maeneo yenye changamoto yanayohitaji kufanyiwa maboresho ili kuweza kufikia dira ya mahakama ya haki sawa kwa wote na kwa wakati.”

Awali Mkurugenzi mtendaji REPOA, Dk Donald Mmari amesema kuwa Mahakama ni mhimili muhimu sana katika dhana ya utawala bora.