Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utaratibu mpya wa kumuaga Magufuli watangazwa, ni kutokana na yaliyojitokeza Dar

#LIVE: Kuagwa hayati John Magufuli Kitaifa Dodoma

Muktasari:

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uzoefu walioupata wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli mkoani Dar es Salaam umewafanya wabadili utaratibu wa kuaga.

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uzoefu walioupata wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli mkoani Dar es Salaam umewafanya wabadili utaratibu wa kuaga.

Amesema awali jeneza lenye mwili wake liliwekwa na watu walipita kuaga lakini katika utaratibu mpya utakaotumika kuanzia leo Jumatatu Machi 22, 2021 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dodoma, mwili utazungushwa uwanjani kama ilivyofanyika jana Dar es Salaam.

Majaliwa ameyasema hayo leo wakati wa shughuli ya kuuaga mwili huo bungeni, “waheshimiwa wabunge leo tumepata nafasi ya kumuaga hapa ni heshima kubwa. Kwa uzoefu tulioupata jana Dar es Salaam watu ni wengi mno waheshimiwa wabunge tusingeweza kupata nafasi hiyo kwa sababu hata ratiba tumeibadilisha kidogo baada ya kuona matamanio makubwa.”

Amesema kuanzia jana utaratibu wa kumuaga wameubadilisha kidogo ili kila mmoja aweze angalau kuona jeneza tu, “kwa kufika na kupata sala lakini baadaye badala ya kwenda kumuaga kwa kumwangalia tutakachofanya ni kuuzungusha mwili angalau mara mbili au tatu uwanjani.”

 “Halafu baadaye tutapita katika mitaa maarufu angalau walio wengi wapate nafasi (ya kumuuaga). Tumeshuhudia watoto wadogo wa umri wa kati, hadi wazee. Tukiruhusu kila mmoja kwenda pale hatutamudu kwa sababu familia imetutaka mwili ulazwe tarehe 26.”