Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Lugola atoa sababu za mauaji ya watoto Njombe

Muktasari:

Mauaji ya watoto wa Njombe yametua bungeni huku Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akisema yanatokana na imani za kishirikina.


Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema imebainika kuwa mauaji ya watoto mkoani Njombe ni ya imani za kishirikina.

Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 30, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa Mufindi Kusini (CCM), Mendrad Kigola.

Mbunge huyo amehoji ni mkakati gani umewekwa na Serikali katika kukomesha mauaji ya watoto katika mkoa wa Njombe ili kurudisha amani mkoani humo.

Akijibu swali hilo, Waziri Lugola amesema tangu juzi Januari 28, 2019 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni yupo mkoani Njombe ambako anafanya vikao vya ndani na kamati za ulinzi ili kutafuta chanzo.

"Tumeshapata orodha ya majina ya wahusika na tumebaini sababu kubwa ni imani za kishirikina, lakini nawaonya wote wanaohusika kuwa wasitingishe kibiriti katika serikali ya Rais John Magufuli, watashughulikiwa," amesema Lugola

Waziri amesema Serikali iko macho na itaendelea kuwa macho katika kuwalinda watu wake na vyombo vya ulinzi havitalala.