Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Rayvanny ang’ang’aniwa Basata, Babu Tale, Fella waingia kumnasua

Muktasari:

Mwanamuziki Rayvanny amekuwa akihojiwa na Basata kwa zaidi ya saa mbili

 


Kikao kati ya baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na msanii Rayvanny kimeonekana kuwa kizito baada ya mameneja wawili wa lebo ya WCB kuingia muda huu kwa kile kinachoonekana kuongeza nguvu.

Mwandishi wa MCL Digital aliyepiga kambi katika ofisi za Basata zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam, amewashuhudia mameneja hao Babu Tale na Mkubwa fela wakiwasili saa mbili baada ya kikao kati ya msanii huo kuwa tayari kimeshaanza

Wakati Babu Tale aliwasili saa 7:19 mchana,  Mkubwa Fela aliwasili saa 7:28 na kuungana na kina Rayvanny katika mahojiano na baraza hilo katika ofisi ya Katibu wake, Godfrey mngereza.

Baada ya kuingia vigogo hao walitoka nje ya chumba cha ofisi hiyo na kuanza kujadiliana wenyewe kwa zaidi ya dakika 20.