Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vurugu Kubwa Iringa, Polisi na wananchi wapambana.

Barabara ya Iringa_ Morogoro - Dar es Salaam ikiwa imefungwa kwa kuchoma moto matairi ya magari. 

Muktasari:

Zipo taarifa za kutokea kwa vurugu kubwa katika eneo la Ilula mkoani Iringa.Taarifa zinadai kuwa vurugu hizo ni kati ya jeshi la polisi na wananchi wa kawaida ambao wamefunga njia kwa kuwasha moto wa matairi ya gari.

Zipo taarifa za kutokea kwa vurugu kubwa katika eneo la Ilula mkoani Iringa.Taarifa zinadai kuwa vurugu hizo ni kati ya jeshi la polisi na wananchi wa kawaida ambao wamefunga barabara kwa kuwasha moto wa matairi ya gari.

Aidha taarifa kutoka kwenye eneo la tukio zinaendelea kueleza kuwa hadi sasa magari manne ya Polisi na Pikipiki moja vimechomwa moto, huku basi linalofahamika kwa jina la Nyagawa linalosafirisha abiria kutoka Njombe kuja Dar es Salaam likiwa limevinjwa vioo vyote.

Taarifa hizo zinadai kuwa tayari polisi wa kutuliza ghasia FFU wameshafika eneo la tukio na kufanikiwa kwa sehemu kutuliza ghasia hizo, na kwamba magari yanayokuja Dar es Salaam na mikoa mingine yameshaanza safari zake.

Ungana nasi baadaye kwa taarifa zaidi