Vyanzo vya maji vyakauka Handeni

Muktasari:
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, walisema tatizo hilo linaonekana kuwa sugu wilayani humo.
Handeni. Vyanzo vya maji katika Halmashauri ya Mji Handeni vinadaiwa kukauka.
Hayo yalisemwa na wakazi wa Halmashauri hiyo ambao wamewataka viongozi kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo hilo mapema kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, walisema tatizo hilo linaonekana kuwa sugu wilayani humo.
Muuza maji, Ally Sabuli alisema imewabidi kuchimba visima pembeni mwa bwawa lililokuwa chanzo kimojawapo kilichokauka ili kupata maji, kwani vyanzo vingine vipo mbali na hawawezi kuvifikia.
Mbunge wa Handeni Mjini, Omari Kigoda alisema tayari Sh1.13 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alifanya ziara hivi karibuni ofisi ya Mamlaka ya Maji safi Handeni (Huwasa) na kuiagiza iboreshe huduma zake, ili kuwapatia wananchi maji kutoka visima vya Nderema.