Waanzisha mfuko kusaidia watakaofiwa na wazazi kuendelea kusoma
Mgeni rasmi, Frank Mang'ati akimkabidhi mwendeshaji mfuko Amos Sollo kiasi cha fedha kilichopatikana baada ya kufanyika harambee
Muktasari:
- Shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 500, wamekubaliana na wazazi kuchanga Sh5000 kila mwezi sawa a Sh60,000 kwa mwaka.
Dar es Salaam. Shule ya Mount Thomas, iliyopo Gongo la amboto jijini hapa imeanzisha mfuko maalum ambao lengo lake ni kusaidia watoto waliofiwa na wazazi wao na ambao watafiwa na wazazi wao wakiwa bado wanasoma shuleni hapo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk Charles Mwansasu, katika harambee ya kuchangia mfuko huo.
Dk Mwasasu alisema wamekuja na mfuko huo ili kuwafanya watoto hao kuendelea kusoma shuleni hapo mpaka watakapomaliza kama zilivyokuwa ndoto za wazazi wao wakiwa hai.
"Haipendezi kuwaacha watoto hawa kwenda kutafutiwa shule zingine ambazo hazikuwa ndoto za wazazi,ndio maana tumekuja na mfuko huu ili wasijisikie vibaya kuwa baada ya wazazi kuondoka maisha yao yamebadilika hadi kwenye kupata elimu,"alisema Dk Mwansasu.
Lakini pa wamekuwa wakiwakaribisha wadau wengine kuchangia mfuko huo.
Mfuko umeanza Aprili mwaka huu na mpaka sasa una watoto sita unaowasaidia na wawaili katu yao walikuwa wameshatolea na walezi wao shuleni hapo hivyo wakafanya kuwarudisha
Amos Sollo, Mwendeshaji wa mfuko huo, alisema wameamua kuja na wazo hilo kwa kuwa sio walezi wote kwamba hawataki kuwasomesha shule hizo binafsi bali baadhi unakuta kweli hawana uwezo.
Aidha Sollo alisema baadaye pia mfuko ni kuja kuwasomesha watoto ambao wazazi wao watakuwa wakisumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo saratani au kutumikia kifungo cha muda mrefu kutokana na matatizo ya hapa na pale.
Katika harambee hiyo alisema awali malengo ilikuwa kukusanya Sh9 milioni lakini wamepata ahadi Sh3 milioni na fedha taslim zaidi ya Sh400,000.
"Tunashukuru kwa wote waliojitolea kuchangia lakini naomba niiambie jamii kuwa jukumu la kulea watoto yatima ni la kila mtu kwa kuwa hao ndio viongozi wa siku zijazo katika nchi hii.
Mmoja wa wazazi,Samia Nyaulingo,alisema wazo La kuanzishwa kwa shule hiyo ni nzuri kwa kuwa hakuna mzazi mwenye ahadi na Mungu kujua kama ataweza kumsomesha mtoto wake mpaka mwisho.
Awali mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Kata ya Pugu, Frank Mang'ati, akimwakilisha Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa, amesema wadau wanapaswa kuwaunga mkono walioanzisha mfuko huo kwa kuwa hakuna anayejua nani atakuwa msaada kwa mwingine.I
Mang'ati pia ametaka jamii kuendelea kupewa elimu ya umuhimu wa kiwasaidia watoto yatima huku kwa wale walaiotoa ahadi zao kuhakikisha wanazikamilisha ili mfuko huo uweze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.