Wachangia Sh15 milioni kujenga nyumba za walimu

Muktasari:
- Katika harambee hiyo, Sh10 milioni zilipatikana kati ya Sh25 milioni zinazohitajika kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Butiama. Wananchi wa Kata ya Nyamimange wilayani Butiama wamefanya harambee kwa ajili ya ukamilishwaji wa ujenzi wa nyumba tano za walimu wa Shule ya Msingi Kwisaro ili waweze kuishi karibu na shule hiyo.
Katika harambee hiyo, Sh10 milioni zilipatikana kati ya Sh25 milioni zinazohitajika kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Harambee hiyo imefanyika kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo, John Kerato na wadau wengine wa elimu ili kusaidiana kufanikisha upauaji wa nyumba za walimu.
Mkazi wa kata hiyo, Veronica Cleophace amesema majengo hayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi baada ya kuhamasishana na kuona shida wanayoipata walimu wanaofundisha watoto wao.
“Tumeamua kujenga nyumba hizi tano za walimu ili waishi karibu na shule na waweze kuwafundisha watoto wetu vizuri, kule mtaani wanapata shida ,” amesema Cleophace.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi amesema Serikali itawaunga mkono wananchi hao kwa jitihada zao ambazo tayari wamekwishazionyesha