Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau waitwa kutoa maoni marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari

Muktasari:

  •  Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inawaalika wadau wa sekta ya habari katika majadiliano kuhusu marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.


Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inawaalika wadau wa sekta ya habari katika majadiliano kuhusu marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.

Majadiliano hayo yatafanyika Agosti 11 – 12, 2022 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupokea maoni yao yatakayowezesha kufanyika kwa marekebisho ya baadhi ya vifungu katika sheria hiyo.

Kwa mujibu wa barua kutoka wizarani kwenda kwa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya habari, taasisi hizo zimeombwa kuteua mjumbe mmoja atakayekwenda kuwasilisha maoni yao kwenye majadiliano hayo.

Taasisi zilizoalikwa kutoa maoni ni pamoja na Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Baraza la Habari (MCT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Misa-Tanzania, Jamii Media na Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari (Jowuta).

“Kutokana na umuhimu wa sheria hii katika kusimamia tasnia ya habari hapa nchini, na kwa kuwa taasisi yako ni muhimu katika utekelezaji wa sheria hii, inaombwa kuteua mjumbe mmoja atakayeungana na wajumbe wengine katika majadiliano yatakayofanyika kati ya serikali na wadau kuhusu maeneo ya sheria hiyo yaliyopendekezwa kufanyiwa marekebisho au kufutwa,” inaeleza barua hiyo.

Tangu kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari, wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao na kuibua upungufu na changamoto mbalimbali ambazo zinaonyesha kuwakwaza katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Moja ya mambo ambayo wadau wanataka yarekebishwe kwenye sheria hiyo ni pamoja na kuuanganishwa kwa taasisi mbalimbali ambazo zitasimamia waandishi wa habari na kuundwa chombo kimoja kitakachojulikana kama Baraza Huru la Vyombo vya Habari.

“Tunataka Bodi ya Ithibati, Mfuko wa Mafunzo na Baraza Huru la Vyombo vya Habari chini ya sheria hii, viunganishwe na kuwa chombo kimoja ambacho ni Baraza Huru la Vyombo vya Habari,” anasema mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile.