Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wakutana kitathmini lishe

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Danstan Kyobya (katikati), akizungumza na wadau mbalimbali wa lishe wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara wakati wa kikao cha tathmini ya lishe kilichofanyika hivi karibuni. Picha na Hamida Shariff

Muktasari:

  • Kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Danstan Kyobya kimejadili tathmini ya nusu mwaka wa utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha Julai 2024-Juni 2025 ambapo miongoni mwa mada zilizowasilishwa na wataalamu ni taarifa iliyoonesha maendeleo yaliyofikiwa katika kutoa elimu ya lishe kwa jamii.

Morogoro. Tathmini ya mapambano dhidi ya udumavu na upungufu wa lishe bora hasa kwa watoto chini ya miaka mitano na wajawazito, imebaini uwepo wa changamoto kadhaa ikiwamo uelewa mdogo wa wazazi na walezi.

Hayo yamebainika katika kikao cha viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, wataalamu kutoka sekta mbalimbali pamoja na wadau wa lishe kuhusu tathmini ya nusu mwaka wa utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha Julai 2024-Juni 2025 kilichofanyika leo Mkuu wa Wilaya ya , Dunstan Kyobya akiwa mgeni rasmi na mwenyekiti wa kikao.

Changamoto zilizobainika ni uhitaji wa nguvu ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi hususani wazazi na walezi wa wanafunzi kuhusu matumizi ya vyakula vyenye virutubisho, ukosefu wa rasilimali za kutosha na changamoto za kiafya zinazochangia udumavu.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa Wilaya Kyobya amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa kwa wazazi na walezi wa wanafunzi kuchangia lishe shuleni.

Kyobya amesisitiza mshikamano kwenye sekta zote, na kusema kuwa mapambano ya lishe si jukumu la sekta ya afya pekee, bali yanahitaji ushiriki wa kilimo, elimu, maji na jamii kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Pilly Kitwana amewahimiza wataalamu na wadau kuongeza ubunifu na mikakati ya kuhakikisha wananchi wanapata lishe bora kupitia uzalishaji na matumizi ya nishati, barabara, maji pamoja na mazao yanayopatikana ndani ya jamii.


Miongoni mwa mada zilizowasilishwa na wataalamu ni taarifa iliyoonesha maendeleo yaliyofikiwa katika kutoa elimu ya lishe kwa jamii, upatikanaji wa chakula bora na utekelezaji wa miradi ya kuongeza kipato kwa kaya.

Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Ifakara katika eneo la lishe, baadhi ya wadau wameamua kuchukua hatua madhubuti kwa kuimarisha ushirikiano wao.

Ushirikiano huu unalenga kuhakikisha afua za lishe zinatekelezwa kikamilifu na kufuatiliwa kwa karibu ili kubaini mafanikio na changamoto zinazojitokeza.

Aidha, juhudi hizo zinajumuisha kupeleka elimu ya lishe kwa wananchi wote, kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu mlo bora na umuhimu wa lishe sahihi kwa afya. Hatua hii inalenga kupunguza viwango vya udumavu kwa watoto na kuimarisha afya ya jamii kwa ujumla, sambamba na kukuza maendeleo endelevu katika eneo la Ifakara.