Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wataka 'Vicoba' vifadhili bima ya afya kwa wote

Muktasari:

  • Katika kuhitimisha mkutano wa 10 wa Afya Tanzania (THS) wadau wa masuala ya afya nchini, wamepaza sauti wakisema Serikali inapaswa kutafuta mbinu mbalimbali kufadhili Huduma ya Afya kwa Wote (UHC) pasipo vikwazo vya kiuchumi ili kufikia mwafaka wa muswada wa sheria uliosua sua kwa muda mrefu.

Dar es Salaam. Serikali imetakiwa kutafuta mbinu mbalimbali zikiwemo benki za jamii za vijiji 'Vicoba' kufadhili huduma ya bima ya afya kwa wote (UHC), inayosubiriwa kwa muda mrefu ili kuhakikisha uendelevu wake, wadau wameshauri.

Ushauri huo unakuja wakati muswada wa bima ya afya kwa wote ukiwa bado unaendelea kukwama, tangu uliposomwa katika bungeni kwa mara ya kwanza Septemba 23, 2022 na kwenda kujadiliwa katika kamati ya bunge ambapo Februari mwaka huu ukakwama kusomwa kwa mara ya pili.

Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 5, 2023 kwenye majadiliano katika siku ya mwisho ya Mkutano wa 10 wa Afya Tanzania (THS) ambapo watafiti, madaktari na wadau wa mashirika mbalimbali ya afya wameshauri mbinu hiyo itumike.

Wadau hao wamesema kuwa kuna haja ya kuwepo kwa mbinu mbalimbali za ufadhili ili kujenga msingi imara wa utekelezaji wa muswada huo kabla ya kupitishwa na kuwa sheria.

Akizungumzia hoja hiyo Mkurugenzi wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wizara ya Afya, Dk Ahmad Makuwani amesema kuna haja ya wadau binafsi na wa umma kujadili pamoja njia za ufadhili kabla ya muswada huo kuanza kutumika.

"Kwa mfano tunaweza kutumia maliasili ambazo tunazo kufadhili muswada huo lakini pia tukachanganya na vyanzo vingine ili kuhakikisha uendelevu," amesema.

Ameongeza kuwa pia kuna fursa katika benki za jamii za vijiji 'vikoba' ambazo zikitumiwa vizuri zinaweza kusaidia kugharamia bima ya afya.

"Tunahitaji kutoa elimu lakini pia kuja na njia nyingi za ufadhili na kuna fursa katika vikoba ambazo zikianzishwa vizuri zinaweza kufadhili muswada huu," amesema.

Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe, Ofisi ya Rais, Mamlaka ya Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk Ntuli Kapologwe amesema ipo haja ya kufikia maelewano ya pamoja kwa wadau kuhusu namna ya kugharamia muswada huo na kuwa endelevu kama ilivyokusudiwa.

Amesema itakuwa haina maana kuzindua sera hiyo na kuiacha isambaratike kutokana na matatizo ya kifedha.

Amesema huduma ya afya kwa wote itakuwa chombo muhimu cha kuwezesha uimarishaji wa utoaji wa huduma ya afya ya msingi na kuongeza kuwa lengo liwe namna ya kuwafanya Watanzania kulipia bima ya afya.

Dk Kapologwe amesema kuwa Watanzania wengi hawana utamaduni wa kuweka kipaumbele cha bima ya afya katika bajeti zao, jambo ambalo alisema linaweza kuathiri uendelevu wa bima kwa wote.

Amesema chanzo kingine muhimu cha fedha ambacho kinaweza kuwa muhimu katika ufadhili wa bima ya afya ni maliasili ambayo ikiwekwa katika muktadha inaweza kusaidia.