Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara walia mahindi kuzuiwa Kenya

Wafanyabiashara walia mahindi kuzuiwa Kenya

Muktasari:

Wafanyabiashara wa mahindi wa Kenya na Tanzania, wameziomba Serikali za pande zote mbili kumaliza mgogoro wa zuio la mahindi kwenda nchini Kenya kwani linaathiri biashara.

Arusha. Wafanyabiashara wa mahindi wa Kenya na Tanzania, wameziomba Serikali za pande zote mbili kumaliza mgogoro wa zuio la mahindi kwenda nchini Kenya kwani linaathiri biashara.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema tangu kuwekwa kwa zuio hilo kwa madai ya mahindi ya Tanzania kuwa na sumukuvu, wanapata hasara na bei inazidi kushuka.

Julius Njoroge mfanyabiashara kutoka Kenya, alisema huja nchini kununua mahindi na kuyapeleka Kenya baada ya kupewa mikopo ya muda mfupi na taasisi za fedha lakini mambo yamekuwa magumu kipindi hiki wanacholazimika kuegesha magari katika mpaka wa Namanga na kulipa dola 200 kila siku.

Mfanyabiashara wa mahindi katika Soko la Kilombero jijini Arusha, John Loshiye alisema bei imeshuka kutoka Sh80,000 kwa gunia moja hadi Sh60,000 katika kipindi hiki cha zuio.

“Hakuna soko la mahindi, bei itaendelea kushuka, wafanyabiashara tutapata hasara na wakulima pia kwani sasa wanauza chini ya Sh50,000 kwa gunia,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Wiwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) mkoani Arusha, Walter Maeda ameissitiza umuhimu wa kuumaliza mgogoro uliopo ili kuruhusu biashara ya mazao kati ya Kenya na Tanzania.

Nchi hizi mbili majirani amesema zinategemeana kwa kiasi kikubwa hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha biashara inafanyika vizuri kwa ajili ya ustawi wa wananchi wake hasa kw akuzingati amahitaji ya chakula nafuu ndio njia pekee itakayosaidi akupambana na maradhi yatokanayo na lishe duni.

Mwenyekiti wa taasisi zinazosafirisha bidhaa kwenda nchini Kenya katika mpaka wa Namanga, Daniel Wainama aliiomba Serikali yake ya Kenya kusitisha zuio la mahindi kutoka Tanzania kwani linaathari kubwa kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili.

“Kawaida wafanyabiashara wa Kenya ndio huenda Tanzania kunnua mahindi na kuyaleta nchini kwa miaka mingi sasa hili agizo sio tu linawaathiri wao hata sisi ambao tunafanyakazi ya kuingiza mizigo Kenya,” alisema Wainama.

Hata hivyo, mkaguzi wa mazao wa Mamlaka ya Kilimo na Chakula Kenya, Calistus Efuko alisema Serikali imeweka zuio kwa mahindi kutoka Tanzania na Uganda kuingia Kenya ili kuepuka sumukuvu kulinda afya za wananchi wanaotegemea chakula hicho kwa kiasi kikubwa.

Mwezi moja uliopita, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Kilimo na Chakula nchini Kenya, Kello Harsama alimwandikia kamishna wa forodha nchini humo, Pamela Ahago kumjulisha kusitishwa kwa uingizaji wa mahindi kutoka Tanzania na Uganda baada ya uchunguzi kubaini si salama kwa matumizi ya binadamu.

Mahindi hayo alisema yamebainika kuwa na viwango vya juu vya sumu ya mycotoxins (sumukuvu) hivyo kutofaa kwa matumizi.

Hata hivyo jitihada zilifanywa kurekebisha sintofahamu hiyo lakini Kenya ikaweka masharti likiwamo la mahindi yote yawe yamepimwa sumukuvu na yawe yamehifadhiwa katika mifuko maalum ya kilo 50 ikionyesha sehemu yalipotoka.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe alisema kutokana na zuio la mahindi ya Tanzania kwenda Kenya, katika mpaka wa Namanga wilayani humo alisema shehena ya mahindi iliyokuwa mpakani imeanza kurejeshwa nchini na kuuzwa nchi nyingine zenye uhitaji zisizo na masharti kama yaliyowekwa na Kenya.