Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafuasi Chadema wafurika kumpokea Lema, ulinzi waimarishwa

Wafuasi wa Chadema wakicheza ngoma wakati wakisubiri kumpokea mbunge wa zamani wa Arusha mjini, Godbless Lema katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Machi 1, 2023

Kilimanjaro. Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka maeneo mbalimbali nchini, wamewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya mapokezi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbless Lema ambaye anatoka nchini Canada.

Lema anatarajiwa kushuka KIA saa 7:10 mchana na Ndege ya Shirika la Ethiopian anawasili nchini baada ya kuwa uhamishoni nchini Canada kwa takriban miaka mitatu.

Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini tayari wamewasili KIA, ambapo pia amewasili Askofu Emmanuel Mwamakula, Sheikh Rajabu Katiba na Mhadhiri maarufu wa vyuo vikuu kadhaa Dk Exavery Rweitama.

Pia wapo waliokuwa wabunge wa majimbo mbalimbali Kanda ya Kaskazini wamewasili, viongozi wa Chadema katika nafasi mbalimbali Mkoa Kilimanjaro na Arusha.

Hata hivyo, polisi wameimarisha ulinzi uwanjani hapo.