Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wahitimu JKT waonywa kulinda viapo vyao

Songwe. Vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika Kambi ya 845KJ lililopo Itaka wilayani Mbozi, Mkoa wa Songwe, wameaswa kutunza afya zao ili waweze kulitumikia vema Taifa ipasavyo.

Mkuu wa kikosi hicho, Luteni Kanali Gervas Chitola amesema hayo leo Jumatatu Septemba 11, mwaka huu wakati akitoa taarifa fupi wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kidato cha sita ambao wamehudhuria mafunzo hayo katika kipindi cha miezi mitatu kwa mujibu wa sheria chini ya operesheni miaka 60 ya JKT.

Chitola amewataka vijana hao kutokwenda kujiingiza katika masuala ambayo yataathiri afya zao badala yake watambue kuwa afya ndiyo mtaji wa kwanza katika maisha ya mtu hivyo inapaswa kutunzwa na kulindwa.

"Kijana mwenye afya njema na nguvu ndiye atakayelijenga na kulilinda Taifa letu, hivyo mjitunze na msiende kujichanganya na makundi ya hovyo bali wakati wote mkilinde kiapo mlichoapa mbele ya Mungu na mbele ya Taifa," amesema Chitola.

Mwakilishi wa kuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia, Jenerali Hassan Mabena amewaasa vijana hao kuheshimu kiapo walichoapa kwani huo siyo wimbo wa kujifurahisha bali ni agano lao na Mungu na nchi, hivyo wawe tayari wakati wote kukitumikia ili Taifa liwe imara kiuchumi na kiulinzi.

Amesema mafunzo ya vijana kwa mujibu wa Sheria yalisitishwa mwaka 1994 kufuatia sababu mbalimbali za kiuchumi duniani na kuanzishwa tena mwaka 2013 kwa kuanza na vijana 5,000 na kwamba hadi Sasa vijana 52,000 wamepata mafunzo hayo nchi nzima.

"Natoa rai kwenu vijana wengi tulipowahoji walisema kabla ya mafunzo haya walikuwa wanalala saa 2 usiku na kiamka saa 4 asubuhi naamini sasa mmepata wepesi mkirudi nyumbani hamtalala tena na msiache kufanya mazoezi," amesema Mabena.

Mkuu wa mkoa Songwe, Dk Francis Michael amesema mkoa unafikiria kuanzisha programu maalumu kama ya BBT ili kutoa fursa kwa vijana waliopitia mafunzo JKT Ili waweze kujiajiri badala ya kutegemea ajira za Serikali.

"Kikubwa kwenu ni kujiepusha na makundi ya hovyo mara mtakaporudi nyumbani bali mkawe mfano nzuri na kuwasaidia Wazazi na walezi kazi za nyumbani," amesema Dk Francis Michael.