Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakili ahoji upelelezi kutokamilika siku 90 kesi ya Mkurugenzi Jatu

Muktasari:

  • Upande wa Utetezi katika kesi inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jatu PLC, Peter Gasaya umedai kesi inayofutwa na kufunguliwa upya kwa makosa yaleyale upelelezi uwe umekamilika ndani ya siku 90.

Dar es Salaam. Upande wa Utetezi katika kesi inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jatu PLC, Peter Gasaya (33) umedai kuwa mwongozo wa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) unasema kesi haiwezi kuletwa mahakamani bila ya upelelezi kukamilika.

Gasaya anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Aprili 11, 2023 mshtakiwa huyo alifutiwa kesi ya jinai namba 207/2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya DPP kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo lakini muda mfupi alikamatwa tena na kufunguliwa upya mashtaka yale yale mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate

Wakili wa Utetezi, Nafikire Mwambona alidai hayo leo Oktoba 9, 2023 wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa kuwa muongozo wa DPP unaeleza kesi ikifutwa haiwezi kuletwa mahakamani hapo bila ya kukamilisha upelelezi.

"Upelelezi ukamilike ndani ya siku 90 lakini tangu shauri hili lifikishwe mahakamani hapa upelelezi hadi leo hii haujakamilika," alidai Mwambona.

Mwambona alidai Mahakama hiyo ina nguvu ya kusimamia mwenendo wa kesi hivyo inaweza kutoa maamuzi.

Wakili Kung'e Wabeya aliieleza mahakama hiyo kuwa upande wa mashtaka waliifuta kesi hiyo na wakaifungua tena mahakamani hapo kwa mashtaka yaleyale.

Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 91(3) sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai marekebisho mwaka 2022 shauri hilo lilipaswa kusikilizwa lakini hadi leo hii upande wa mashtaka wanadai upelelezi hawajakamilisha.

Baada ya maelezo hayo Hakimu, Richard Kabate alisema kesi hiyo ni ya uhujumi uchumi yeye hana mamlaka ya kutoa maamuzi yeyote mwa kuwa Mahakama kuu ndiyo yenya mamlaka ya kutoa maamuzi.

Awali, Wakili wa Serikali, Aroun Titus alidai kuwa kifungu cha 91(3) kinataka shauri hilo lisikilizwe lakini kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi hata maelezo ya awali (PH ) yatasomwa katia Mahakama Kuu ya Tanzania.

"Tunakamilisha upelelezi ili mahakama iweze kusikiliza na aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa," amedai Titus.