Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakili akwamisha kesi uvamizi Kanisa RC Geita

Mshtakiwa Elpidius Edward (22) akiwa chini ya ulinzi akisubiri kurejeshwa mahabusu baada ya shauri la kuvamia na kuharibu mali ndani ya Kanisa kuu Jimbo Katoliki Geita kuahirishwa.

Muktasari:

Tukio la kuvamiwa na kuharibiwa mali ndani ya Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki Geita lilitokea Februari 26, 2023.

Geita. Shauri la kuvamia na kuharibu mali zenye thamani ya Sh48.2 milioni ndani ya Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Geita linalomkabili Elpidius Edward (22) mkazi wa mtaa wa Katundu mjini Geita limeahirishwa kutokana na Mwanasheria wa Serikali anayesimamia kesi hiyo kuwa kwenye vikao Mahakama kuu.

Akitoa ombi la hairisho la kesi hiyo namba 62/2023, Wakili wa Serikali, Musa Mlawa ameieleza Mahakama Hakimu Mkazi Geita kuwa ushahidi wa shahidi uliotarajiwa kusikilizwa leo Mei 10, 2023 hautatolewa kwa sababu wakili anayehusika ana majukumu mengine Mahakama Kuu.

‘’Tunaomba kuoangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi,’’ amesema Wakili Mlawa

Kutokana maombi hayo, Hakimu Mkazi Geita, Johari Kijuwile ameahirisha shauri hilo hadi Mei 24, 2023 itakapokuja kwa ajili ya upande wa mashtaka kuendelea na ushahidi.

Katika shauri hilo, mshatakiwa Elpidius anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo la kuingia kwa jinai ndani ya jengo la Kanisa Kuu jimbo la Geita kinyume na kifungu cha 294 (1) na (2) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Katika shtaka la pili mshtakiwa huyo anadaiwa kuharibu mali zenye thamani ya Sh48.2 milioni kinyume na kifungu namba 226 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mshatakiwa amerejeshwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaotakiwa kusaidi hati ya fedha taslimu Sh24.1 milioni au mali isiyo hamishika yenye thamani hiyo.