Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi Chunya wapatiwa taulo za kike

Chunya. Wanafunzi wa kike 52 kati ya 350 wa shule ya sekondari Sangambi wilayani chunya mkoa wa Mbeya wameacha masomo  kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo ukosefu wa taulo za kike na chumba cha kujisitili  wanapokuwa hedhi.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu Diana Kalinga amesema hayo leo Jumatano Machi 8, 2023 akisoma taarifa iliyoandaliwa na shule hiyo mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya utoaji wa taulo za kike iliyoanzishwa na mke wa Mbunge wa Jimbo la Lupa, Veronica Masache ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mwanamke duniani.

“Shule yetu ina wanafunzi 350 wa kike  kati ya hao zaidi ya wanafunzi 52 wameacha masomo kutokana na sababu za kibailojia na kuishia mitaani jambo ambalo linawakosesha haki ya kupata elimu” amesema.

Amesema kuwa upatikanaji wa taulo za kike utasaidia kusoma kwa bidii na kupunguza tatizo la utoro na wanafunzi wa kike  na kuomba Serikali kuunga mkono juhudi za wadau wanaojitoa kusaidia watoto wa kike.

Kwa upande wake Veronica Masache amesema kuwa kutokana na changamoto ya hedhi zisizo salama  na kulazimika kuanzisha kampeni  maalum ya kugawa taulo za kike katika shule zote za msingi na Sekondari wilayani humo

“Tumebaini kuwepo kwa changamoto kwenye shule pembezoni hivyo nimewiwa kulifanya hilo lengo ni kuona mtoto wa kike anakuwa huru na kupata elimu bora ili kuzalisha wasomi watakaokuja kulisaidia taifa kwa kuzalisha wasomi” amesema.

Veronica amesema kuwa wataendelea kuwekeza kwenye sekta ya elimu kwa kumjali mtoto wa kike kwa kutambua kuwa ukimuwezesha mtoto wa kike umelikomboa taifa

“Nikiwa kama mama natambua changamoto za watoto wakiwa kwenye hedhi wanakuwa sio wasikivu kwenye masomo hivyo upatikanaji wa taulo za kike utawezesha  kusoma kwa bidii na kupunguza tatizo la utoro mashuleni,"

Mwalimu wa kike katika Shule hiyo, Jackline Challes amesema kuwa ukosefu wa taulo za kike umechangia wanafunzi kuugua magonjwa ya kuambukiza  kama fangasi na ukosefu wa chumba maalum cha kujisitili.

“Idadi kubwa ya wanafunzi wa kike wanaugua magonjwa ya kuambukizwa ikiwepo utoro kwani mwa mwaka mwanafunzi wanashindwa kuhudhuria masomo kwa kipindi cha miezi mitatu na kusababisha kuishia mitaani ” amesema.

Amesema wana kila sababu ya kumshukuru mbunge wa Jimbo la Lupa kupitia kwa Mke wake Veronica kwa kuliona hilo na kuwashika mkono watoto wa kike kwa lengo la kuhamasisha suala la elimu kwa watoto wa kike.