Wananchi waja na majibu tatizo la ajira nchini

Muktasari:
- Wananchi wameiomba Serikali kupokea na kuzingatia ushauri unaotolewa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sambamba na na wadau wa elimu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchi na kuwasaidia wahitimu mbalimbali kupata ajira.
Buchosa. Wananchi wamesema njia pekee ni serikali kuanzisha mtaala wa somo la codingi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu ili kupambana na janga la wahitimu mbalimbali wa vyuo vikuu na vyuo vya kati hapa nchini kutembea na vyeti kila kona kusaka ajili bila mafaniko.
Lengo la kuanzishwa somo hili, wananchi wanasema litasaidia wahitimu kujiajiri tofauti na sasa mitaala wanayosoma inategemea kuajiriwa. Hivyo somo hili litakapoazishwa shuleni litapunguza adha ya wahitimu kutembea na vyeti kusaka ajira.
Mchango huo ulitolewa bungeni na Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo wakati akitoa hoja kwenye vikao vya mbunge ambapo aliomba serikali kuanzishwa mtalaa huu ili wanafunzi waendane na soko la ajira ili kuenenda na dunia ya sayansi na teknolojia.
Shigongo amesema ushauri aliutoa kwa serikali kuanzishwa kwa somo la codingi aliiomba serikali kuanzisha somo hilo kwa sababu aliona jinsi wahitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati wanavyosota kusaka ajira bila mafaniko kutokana na sababu hawakuwa na somo la kujitegemea kupata ajira.
Mapema mwaka 2022 mwezi Desemba Rais wa Jamuhuri ya Kenya, Wiliamu Ruto alitangaza Taifa hilo kuanza kufundisha somo la codingi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ili kuendana na soko la ajira hapa dunia.
Anastazia John ameiomba serikali kuangalia na kutathamini michango ya wabunge wakati wanapoishauri serikali kuanzisha jambo ambalo linatakuwa msaada na mkombozi wa katika Taifa.
Mapenda mwaka huu mwezi Februari, Waziri Elimu Sanyansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda wakati akihojiwa na ITV kipindi cha dakika 45 alisema serikali inaangalia namna ya kuanzisha
somo la codingi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu lengo ni kuendana na soko la ajira hapa nchi.
Alisema kuna haja sasa katika mitalaa mipya kuanzisha somo ya codingi mashuleni kuanzia shule za misingi na kuendelea.
"Bunge linapotoa ushauri serikali tunapokea, tumeona tukianzisha mtalaa wa somo la codingi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu tutakuwa tumewasaidia watoto wetu kujiajiri na kuenenda na soko la ajili,” amesema Mkenda.