Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanandoa watimua mbio wakiachiwa huru kesi ya bangi

Washtakiwa Anjimile Chemba wa kwanza kushoto akifuatiwa na Asha Mbuta wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kukimbia baada ya kufutiwa kesi yao ya kusafirisha dawa za kulevya aina bangi gramu 66.70. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Washtakiwa watatu wakiwemo wanandoa waliokuwa wanakabiliwa na shtaka moja la kusafirisha gramu 66.70 za Bangi kinyume cha sharia wameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi na kuwachia huru watu watatu wakiwemo wanandoa waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi gramu 66.70, baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa zaidi ya mara tano mfululizo bila kuendelea na usikilizwa wa upande wa mashtaka.

Sababu nyingine iliyofanya mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo ni kutokana na Serikali kushindwa kupeleka mashahidi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo.

Waliofutiwa kesi na kuachiwa huru na Mahakama hiyo ni Anjimile Chembe (40) na mume wake Shabani Abdallah (48) pamoja na Asha Mbuta (27).

Mbali na kuwafutia, Mahakama hiyo imetoa maelekezo kwa upande wa mashtaka kuwa washtakiwa hao wasikamatwe hadi Serikali ikakapokata rufaa Mahakama Kuu.

Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo umetolewa leo Machi 28, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemarila wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili kuendelea na ushahidi.

"Kesi hii ni ya muda mrefu, ilifunguliwa mahakamani hapa Novemba 21, 2019 ina zaidi ya miaka minne na ni moja ya kesi zilizopo katika mrundikano wa kesi " amesema Hakimu Rugemalira na kuongeza.

"Shahidi wa kwanza alitoa ushahidi wake Novemba 29, 2011 na baada ya hapo ilikuwa ina ahirishwa mara kwa mara na shahidi wa sita ametoa ushahidi wake Januari 30, 2023 na baada ya hapo kesi hii imekuwa ikiahirishwa bila kuendelea zaidi ya mara tano hadi leo"

"Kutokana na hali hii Mahakama haiwezi kuruhusu kesi hii kuendelea na usikilizwaji wakati upande wa mashtaka hawana nia nayo na hawaleti mashahidi, hivyo nawaachia huru washtakiwa wote na wasikamatwe hadi Serikali ikakate rufaa Mahakama Kuu" amesema Hakimu Rugemalira.

Washtakiwa wamefutiwa kesi yao chini ya kifungu 225(4) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), ambacho kinaipa Mamlaka Mahakama ya kufuta baadhi ya kesi zilizozidi siku 60 bila kuendelea na usikilizwaji.

Awali, wakili wa Serikali Mosie Kaima aliieleza mahakama hiyo kuwa shauri hilo limeitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, lakini hakuwa na shahidi na hivyo aliomba mahakaka ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Kaima baada ya kueleza hayo, ndio hakimu alipohoji sababu ya kesi hiyo kuahirisha mara nyingi bila kuendelea na kisha kuandika uamuzi wa kuwafutia kesi.


Washtakiwa watimua mbio baada ya kuachiwa huru:

Ni kama walikuwa hawaamnini kilichotokea mahakamani baada ya Hakimu kutamka kuwa anawaachia huru washtakiwa wote na wasikamatwe, washtakiwa walimshukuru Hakimu kwa kuwafutia kesi huku wakiwa na nyuso za furaha na kuangalia.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kutoka na chumba cha mahakama namba 20, kilichopo ghorofa ya kwanza, walitoka wakikimbia kushuka ngazi na walipofika chini waliendeela kukimbia wakihofu kukamatwa tena.

Hata mshtakiwa Aisha ambaye ana ujauzito mkubwa alionekana kuwa mkakamavu wa kukimbia kushuka ngazi za Mahakama hiyo na hatiamye kukimbia hadi nje ya lango kuu la kuingilia mahakamani huku akiwaeleza wenzake kuwa wasizubae wanawaweza kukamatwa tena.

"Nyie kimbieni mnaweza kukamatwa tena, twendeni tuondoke eneo hilo la Mahakama " alisikika Asha akiwaambia wenzake huku wakiendelea kukimbia kwa spiidi.

Mara ya mwisho, kesi hiyo iliahirishwa Machi 15, baada ya shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi kuwa ana matatizo ya kifamilia na alisafiri kwenda Dodoma.


 Kesi ya msingi:

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo, Novemba 2019, katika eneo la Kipunguni, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa kwa pamoja walikuwa wanadaiwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 66.70, kinyume cha sheria.

Hadi wanafutiwa kesi hiyo washtakiwa wote walikuwa nje kwa dhamana.