Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne matatani kukutwa na shehena ya bangi

Shehena ya dawa za kulevya aina ya bangi zilizokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti, wakitumia mbinu mbalimbali za kuhifadhi vitu hivyo kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.

Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wanne, wakiwemo wanawake wawili, kwa tuhuma za kukutwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya bangi.

Watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti, wakiwemo wanawake wawili waliokutwa wakihifadhi bangi ndani ya masanduku kwenye nyumba yao ya makazi, huku wengine wakinaswa wakisafirisha shehena hiyo kuelekea jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ameeleza hayo leo Jumatano Mei 22, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema katika tukio la kwanza, jeshi hilo linawashikilia Seva Simwinga (29) na Sara Simwinga (35), wafanyabiashara na wakazi wa Mponja, Kata ya Uyole, jijini Mbeya.

Kamanda Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilogramu 320, wakiwa wamehifadhi dawa hizo ndani ya nyumba yao.

Amesema watuhumiwa walikamatwa usiku wa kuamkia Mei 21, 2025, katika operesheni maalumu iliyofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, iliyofanyika katika Mtaa wa Mponja, Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga, jijini Mbeya.

"Baada ya kupekuliwa, walikutwa na magunia manne pamoja na masanduku manne yenye dawa hizo za kulevya, zote zikihifadhiwa ndani ya nyumba yao," amesema Kamanda Kuzaga.

Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia Billy Mtafya (19) fundi magari, mkazi wa Uyole jijini Mbeya na Joseph Nyalusi (25) kondakta wa basi, mkazi wa Dodoma wakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilogramu 30.

Watuhumiwa walikamatwa kati ya Mei 19 na 20, 2025  saa 8:00 usiku katika kizuizi cha Polisi eneo la mpakani katika barabara Kuu ya Mbeya kwenda Mkoa wa  Njombe wilayani Mbarali.

Amesema watuhumiwa  baada ya kupekuliwa walikutwa wakiwa na mabegi manne na sanduku moja yakiwa yamefungwa na mifuko laini, ndani yake yakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

"Watuhumiwa walitumia mbinu ya  kusafirisha kama mzigo katika mabasi mawili tofauti ya abiria,” amesema.

Hata hivyo, watuhumiwa baada ya kuhojiwa wamekiri kuhusika na biashara hiyo ,huku akionya wananchi wanaojihusisha na tabia hiyo kuacha mara moja.

Kuzaga ametoa wito kwa wananchi wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kuacha mara moja, kwani haina nafasi katika jamii.