Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waomba msaada wa Serikali viboko kuvamia makazi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda (aliyevaa miwani) katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Bethany Child Care baada ya kukabidhi zawadi kituoni hapo. Picha na Samirah Yusuph

Muktasari:

Kituo cha Bethany Child Care kipo pembeni mwa Ziwa Victoria katika wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu ambapo kimekuwa hatarini kutokana na viboko kuvamia makazi ya watoto na kuhatarisha maisha yao.

Busega. Uongozi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Bethany Child Care wilayani Busega mkoani Simiyu umeiomba Serikali kuingilia kati changamoto ya viboko wanaotoka ziwani kuvamia makazi yao.

Changamoto ya viboko kuvamia makazi ya watoto kituoni hapo imebainishwa katika taarifa ya kituo hicho iliyosomwa na John Paul leo Desemba 24, 2022.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa viboko wamekuwa wakitoka ziwani na kuharibu mazao pamoja na kusogea karibu na makazi ya watoto nyakati za usiku, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watoto.

“Suruhisho la uvamizi huo ni kujenga ukuta kuzunguka kituo ili kuimalisha ulinzi wa watoto hivyo tunaiomba serikali kutushika mkono ili kufanikisha ujenzi,” amesema John, kijana anayelelewa kwenye makazi hayo.

Kituo cha Bethany Child Care kipo pembeni mwa Ziwa Victoria katika wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu ambapo kinahudumia watoto 148 na wafanyakazi 49 wenye uhitaji pamoja na kuendesha shule ya msingi ambayo watoto waliyopo kituoni na wanaoishi maeneo ya jirani wanaopata elimu bure.

Akiwasilisha salaamu za Rais Samia Suluhu Hassan, mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda ameagiza uongozi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano kwa kituo hicho ikiwa ni pamoja na kutoa hati miliki ya eneo lililojengwa kituo.

“Nitawachangia na viongozi wengine watachangia lakini namuagiza mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi kuchangia ili kufanikisha eneo hili kupata hati miliki kwa mujibu wa sheria pamoja na kutatua kero zilizopo,” amesema Nawanda.

Salamu za upendo za Rais zilizotoleewa kituoni hapo ziliambatana na zawadi ya sikukuu kwa watoto ikiwemo vyakula ili kuhakikisha wanamaliza mwaka kwa furaha na kutambua kuwa serikali inawakumbuka.

Baadhi ya watoto wameeleza furaha yao na kumshukuru Rais Samia kwa kulikumbuka kundi hili.