Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watakaochoma Mlima Kilimanjaro kukiona

Muktasari:

  • Kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kufanya uharibifu wa mazingira na ujangili katika Mlima wa Kilimanjaro.

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameitaka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (Kinapa) kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kufanya ujangili, uharibifu wa mazingira pamoja na kuwasha mioto katika hifadhi hiyo.

Babu ameyasema hayo leo Jumatano, Machi 15,2023, wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa uhifadhi, utalii na mabadiliko ya tabianchi, uliofanyika  katika Ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1973.

Mkuu huyo amesema uharibifu wa mazingira katika msitu unaozunguka hifadhi ya kilimanjaro, unadumaza ukuaji wa kipato cha nchi na kuchochea ongezeko la ukame hivyo ni lazima wahusika wachukuliwe hatua ili kudhibiti tatizo hilo.

"Watu wanaofanya tabia za hovyo kwenye hifadhi wachukuliwe hatua kali, kwa sababu wanahujumu nchi na iwe fundisho kwa watu wengine,"amesema Babu.

Ameongeza kuwa "Wananchi punguzeni mifugo yenu inawazidi na kusababisha muingie ndani ya hifadhi jambo amablo hatutalivumilia hata kidogo.Tunahitaji ushiriki wenu katika uhifadhi wa misitu yetu," amesema.

Awali akitoa taarifa juu ya hali ya uhifadhi na changamoto walizokabiliana nazo katika kipindi cha miaka 50 Naibu Kamishna wa uhifadhi (Tanapa), Asteria Ngaga amesema miongoni mwa changamoto zilizopo ni uwepo wa shughuli za kibinadamu ikiwemo uwashwaji wa mioto mara kwa mara ,uokoataji wa kuni, pamoja na ujangili. 

"Bado tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ujangili wa wanyama pori, kuendelea kwa shughuli za kibanadamu katika msitu kama vile ukataji wa nyasi, uokotaji kuni pamoja na migogoro ya mipaka,"amesema Asteria.

Ngaga ameongeza kuwa utunzaji wa hifadhi ni jukumu la kila mtanzania na siyo taasisi za Tanapa pekee ili kusaidia kuendeleza uhifadhi.