Watanzania sasa kwenda Hong Kong bila karantini

Muktasari:
Dalili njema za kupungua maambukizi ya Uviko-19, baada ya mamlaka za China kupunguza baadhi ya masharti kwa wasafiri.
Dar es Salaam. Kasi ya maambukizi ya Uviko-19 inaonekana kupungua nchini China, baada ya mamlaka za taifa hilo kuondoa baadhi ya masharti kwa wasafiri.
Leo Jumanne, Septemba 27, 2022, Balozi wa Tanzania nchini China, Mberwa Kairuki kupitia ukurasa wake wa twitter ametoa taarifa ya kusitishwa kwa sharti la kukaa karantini kwa wasafiri kutoka nchini.
Awali, kwa atakayetaka kwenda nchini humo alitakiwa kukaa karantini wiki mbili kabla ya baadaye kupunguzwa na kubaki wiki moja.
Lakini, taarifa ya Balozi Kairuki inasema kwa Watanzania watakaosafiri kutoka Tanzania kwenye Hong Kong nchini humo hawatatakiwa kukaa karantini.

"Habari njema kwa Watanzania wenye kuhitaji kwenda Hongkong kwa ajili ya shughuli za uchumi na kijamii. Sasa hawahitajili kufanya karantini," amesema.
Hatua hiyo, Balozi Mberwa amesema gharama za usafiri kwenda China kupitia Hongkong.