Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto 400,000 kupatiwa chanjo ya polio Songwe

Ofisa Uelimishaji toka Wizara ya Afya, Penford Joel

Muktasari:

  • Serikali imesema mikoa sita nchini itatoa chanjo ya Polio ya Matone kuanzia Septemba 21 hadi 24, 2023.

Songwe. Zaidi ya watoto 400,000 wenye umri chini ya miaka 8 Mkoani Songwe wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Polio ya matone ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa kupooza.

Hayo yameelezwa leo Septemba 16, 2023 na ofisa uelimishaji toka Wizara ya Afya, Penford Joel alipozungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Songwe, akisema Serikali imeamua kutoa chanjo hiyo kufuatia kisa kimoja cha ugonjwa wa polio kujitokeza Mkoani Rukwa mwaka huu.

Amesema licha ya kuwa chanjo hiyo imeendelea kutolewa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya lakini inaonesha baadhi ya magonjwa yamekuwa yakijirudia kutokana na mwingiliano wa watu na hasa maeneo ya mipaka na nchi za jirani.

"Ratiba ya kampeni ya chanjo itaanza Septemba 21 hadi 24 kwa awamu ya kwanza na kwamba itahusisha mikoa sita ya Katavi, Kigoma, Kagera, Rukwa, Songwe na Mbeya," amesema Joel.

Amesema katika mkoa wa Songwe watoto wapatao 402,644 wenye umri wa kuanzia miaka sifuri hadi minane watachanjwa kupitia operasheni hiyo ambayo itakuwa nyumba kwa nyumba.

Kwa upande wake mkazi wa Nselewa wilayani Mbozi Gloria Mwampashe amesema wakati wa uendeshaji wa chanjo hizo uzingatie makundi yote ya kijamii na hasa kundi la watoto ambao hawajulikani makazi yao lakini ni wenye umri mdogo.

"Tunawaona mitaani baadhi ya watoto mitaani ambao hawajulikani wanakotoka ambao nao wapo hatarini kuambukizwa maradhi mbalimbali,” amesema Gloria.