Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto milioni 3 wanakabiliwa na hali ya udumavu

Muktasari:

  • Zaidi ya watoto milioni 3 nchini wanakabiliwa na hali ya udumavu, takwimu zinaonyesha kuwa udumavu umepungua kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi asilimia 32 mwaka 2018.

Bariadi. Zaidi ya watoto milioni 3 nchini wanakabiliwa na hali ya udumavu, takwimu zinaonyesha kuwa udumavu umepungua kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi asilimia 32 mwaka 2018.

Taarifa ya wizara ya kilimo iliyosomwa na Dk Mashaka Mdangi leo Oktoba 11,2022 katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya chakula nchini yaliyofanyika mjini Bariadi ambapo amesema umepungua kutoka asilimia 3.8 mwaka 2014 hadi asilimia 3.5 mwaka 2018.

Amesema pamoja na kuwa nchi yetu imejaaliwa kuwa na uwezo wa kuzalisha mazao mbalimbali ya chakula bado hali ya lishe nchini sio nzuri japo kuwa taarifa zinaonyesha kuna maendeleo mazuri katika kupunguza utapiamlo.

"Hali hii imesababishwa kwa kiasi kikubwa na jamii nyingi kutokutambua umuhimu wa kula mlo kamili wenye mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya vyakula ili kuwa na afya bora,".

Aidha ameainisha kuwa tathmini imeonyesha kuwa uzalishaji wa mazao ya  chakula unatarajiwa kufikia kiasi cha tani 17.4 milioni Kwa mlinganisho wa nafaka ambapo tani 9.4 milioni ni mazao ya nafaka na tani 7.9 milioni ni mazao yasiyonafaka.

Uzalishaji wa msimu wa 2021/2022 utapungua kwa kiasi cha tani 1.02 milioni sawa na asilimia 5.5 ikilinganishwa na tani 18.4 milioni msimu wa mwaka 2020/2022.

Akifungua maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuthamini hali ya chakula nchini na nje ya nchi na kuhamasisha uzalishaji na upatikanaji wa chakula bora, salama na cha kutosha kuanzia ngazi ya kaya hadi kitaifa.

"Kuongeza jitihada na mbinu za kutokomeza njaa, utapiamlo na hatmaye kuondoa umasikini, kuiaminisha mikakati thabiti ya kuhakikisha Kila mtu anapata chakula bora na cha kutosha wakati wote.

Pamoja na kuelimisha wananchi kuondoka na mila potofu zinazozuia baadhi ya jamii kula aina fulani za vyakula, " amesema Nawanda.

Kwa upande wa hali ya mahitaji ya chakula nchini katika mwaka 2022/2023 ni tani 15.07 milioni ambapo tani 9.5 milioni ni mazao ya nafaka na 5.5 milioni ni mazao yasiyo ya nafaka kwa kulinganisha uzalishaji wa mahitaji nchini inatarajiwa kuwa utoshevu kwa asilimia 115.

Pamoja na upungufu wa uzalishaji kwa upande wa mazao ya nafaka utengamano wa hali ya chakula nchini utaendelea kuwepo kutokana na ziada inayotokana na mazao yasiyo nafaka kiasi cha tani 2.3 milioni.