Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto waishio mazingira magumu wapungua kwa asilimia 27

Muktasari:

  • Ikiwa dunia inaadhimisha siku ya watoto wa mitaani leo Aprili 12, watoto wa mitaani wamengua kwa asilimia 27 kwa mujibu wa Ustawi wa Ja mii nchini.

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiadhimisha siku ya watoto wa mitaani leo Aprili 12, idadi ya watoto wa mitaani imetajwa kupungua katika mikoa ambayo inaongoza kwa idadi kubwa ya watoto hao hapa nchini.

Utafiti uliofanywa na Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii umeonyesha watoto wa mitaani wamepungua kwa asilimia 27 mwaka 2020/2021 ikilinganishwa na mwaka 2017/2018 ukiwa umefanyika katika mikoa ambayo ina idadi kubwa ya watoto hao ambayo ni  Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Arusha na Iringa.

Katika utafiti huo serikali ilibaini uwepo wa jumla ya watoto 6393 (Wavulana 4865, Wasichana 1528) mwaka 2017/2018 huku Mwaka 2020/2021 ikibaini uwepo wa jumla ya watoto 4,383 (Wavulana 3508, Wasichana 875).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 12 jijini hapa, Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii nchini, Baraka Makona amesema utafiti huo umebaini sababu kadhaa za uwepo wa watoto hao wa mitaani zikiwemo malezi duni katika familia yasiyojali mahitaji na haki za watoto.

Nyingine ni umasikini wa kipato katika familia, vifo vya wazazi au walezi pamoja na vitendo vya ukatili/unyanyasaji Majumbani

“Kila mtu ana kitu anachokipenda, mtoto anaweza kutoroka shule kwa sababu kuna kitu anakipenda, kwa hiyo hata ukimrudisha shule hawezi kukubali, kwa hiyo wengine tunawapeleka Veta kulingana na matakwa yao," amesema Makona.

Makona amesema wapo watoto ambao walimaliza darasa la saba na walikataa kuendelea na shule na wanaendelea na shughuli zao ambazo zinawaingizia vipato lakini wengi wanaendelea na shule.

"Wengine tunawachukua tunakaa nao kwa kuwapeleka kwenye vituo vya kulelea watoto ambavyo viko 426 kote nchini vya serikali pamoja na mashirika binafsi ambapo huko huendelea na masomo pia," alisema Makona.

Aidha Makona amebainisha miongoni mwa jitihada zilizofanyika na kusababisha kupungua kwa idadi ya watoto hao zikiwemo Serikali za Mitaa kuanzisha sheria za kukabiliana na changamoto ya uwepo wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Nyingine ni kutolewa kwa elimu ya malezi na makuzi kwa wazazi na jamii kwa ujumla kupitia majukuwaa mbalimbali huduma inayotolewa kwa uhakika na Maafisa Ustawi wa Jamii nchini.