Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu wasijulikana wadaiwa kumuua mfanyabiashara Moshi

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa.

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Juni 25, 2024 amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia

Moshi. Mfanyabiashara wa ndizi Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Christina Kisima (63) amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu butu kichwani na watu wasiojulikana.

Chanzo cha kifo hicho kinadaiwa ni mgogoro wa ardhi baina yake na mtoto wa mwanamume aliyezaa naye.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Njari, Wilaya Moshi, anadaiwa kuuawa usiku wa kuamkia Juni 23 2024, wakati akitoka kwenye shughuli zake, akielekea nyumbani.

Inadaiwa baada ya mauaji hayo, watuhumiwa waliutelekeza mwili wa marehemu uchochoroni ukiwa mtupu na majeraha sehemu mbalimbali za mwili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Juni 25, 2024 amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia.

Amedai kuwa Christina alikuwa akigombea kipande cha ardhi na mtoto wa mwanamume aliyezaa naye.

"Mnamo juni 23, saa 1:36, asubuhi, Christina Kisima aliuawa baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na kitu butu kichwani na watu wasiojulikana usiku akitoka kwenye matembezi maeneo ya jirani akielekea nyumbani kwake,” amesema.

Kamanda Maigwa amesema kabla ya kifo chake, Juni 22, saa 3:00 usiku, Christina alionekana nyumbani kwa mmoja wa majirani zake akinywa pombe na wenzake.

"Mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha mawili usoni na matano kisogoni, kiini ni ugomvi wa familia, marehemu inasemekana alikuwa anagombea kipande cha shamba na mtoto wa mwanamume aliyezaa naye na wauaji walimvizia wakati anarudi nyumbani peke yake ndiyo wakamshambulia,” amefafanua  Kamanda Maigwa.

Amesema juhudi za kuwatafuta watuhumiwa waliohusika na tukio hilo zinaendelea na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa uchunguzi zaidi.

Mtoto wa marehemu, Evarist Tete amesema siku ya tukio mama yake alikuwa ametoka kwenye shughuli zake za kuuza ndizi Moshi Mjini.

Amesema alipata taarifa za mwili wa mama yake kukutwa umetupwa kwenye njia ambayo huitumia kupita kufika nyumbani kwao.

"Mama alitoka kwenye biashara yake ya ndizi akapitia sehemu, sasa muda aliotoka hapo ulikuwa siyo rafiki sana na alishazoea kujiamini kuwa hakuna kinachoweza kumpata njiani, ndipo akavamiwa na watu ambao hatujawajua mpaka sasa maana alikuwa mwenyewe," amesimulia mtoto huyo.

Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa kijiji hicho, Aloyce Shau amesema taarifa zilizopo zinadai kuwa kabla ya kuuawa kwa mwanamke huyo, alibakwa.

"Huyu mama inavyoelezwa ni kwamba alitoka kwenye shughuli zake za kuuza ndizi na kupitia kwa jirani ambako kulikuwa na sherehe, sasa wakati akirudi nyumbani usiku, ndipo alipovamiwa na watu hao na kuuawa, mwili wake ulikutwa asubuhi na watu ambao walikuwa wanaenda kanisani.